Matokeo ya Nani Mtani Jembe kuanza kutangazwa leo

1Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akiwakabidhi wafanyakazi wa TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuwashinda wanaoshabikia Yanga katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager inawashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga. 3Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Mariam Martin zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya 5Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. 7Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Bahati Msokwa zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. 8Wafanyakazi wa TBL Mbeya Frank Kasege (kushoto) na Bahati Msokwa (kulia) wakishindana kupiga danadana katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya 9Wafanyakazi wa TBL Mbeya Frank Kasege (kushoto) na Andrew (kulia) wakishindana kupiga danadana katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. 12Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya 13Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya 15Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akishangilia na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuibuka washindi katika shindano la kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. 16Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akitambulisha kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa TBL Mbeya mwishoni mwa wiki.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager itaanza kutangaza matokeo ya kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoshirikisha mashabiki wa timu kubwa nchini za Simba na Yanga kupitia vyombo vya habari kila siku.
Meneja wa Bia ya hiyo, George Kavishe aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Shindano hilo kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika kwenye kiwanda cha bia cha TBL Jijini Mbeya.
Katika shindano hilo Kilimanjaro inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.
Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.
Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 1,000 kutoka kwa Simba.
Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku kuanzia leo Jumatatu hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.
Kavishe alisema kuwa mashabiki watakaoshiriki kwenye shindano hilo kila siku pia watanufaika kwa kuchaguliwa watu 400 watakaokuwa wametuma mara nyingi zaidi ambao pia watazawadiwa shilingi 5000 kila mmoja na kufanya kiasi cha fedha zinazokwenda kwa mashabiki kuwa shilingi milioni mbili kila wiki.
Katika uzinduzi huo wa Nani Mtani Jembe kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Simba iliwakilishwa na Mwenyekiti wake Ismail Aden Rage na Yanga iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Yanga Mohamed Bhinda.
Mashabiki wanaweza kufatilia matokeo kila dakika kupitia tovuti maalum ya Nani Mtani Jembe ambayo ni https://cms.rasello.com/kili.

Comments

Popular posts from this blog