GARI YATEKETEA KWA MOTO MBELE YA ASKARI WA USALAMA BARABARANI

Gari aina ya HIACE inayofanya safari zake mkoani kilimanjaro katika root ya Moshi-Marangu kila siku, Juzi asubuhi tarehe 13/10/2013 Majira ya saa mbili asubuhi iliwaka moto maeneo ya YMCA ikiwa inatokea Marangu na abiria wapatao 18, ila hakuna madhara kwa abiria.
Ikiwa katikati ya mji kabisa pasipo kuwa na msaada wa haraka kutoka FIRE iliyojirani na eneno la tukio na hata msaada wa  askari wanaosaidia katika maeneo hayo,
kwa mujibu wa Mwanahabari wetu FRANK aliyeshuhudia tukio ilo, hapakuwa na msaada wa haraka toka FIRE mpk baada ya dakika kadhaa kuteketea kwa gari hilo ndio walipokuja kusaidia.
 Askari wa barabarani wakigeuka kuwa waandishi wa habari na kusahau majukumu yao kama wanavyoonekana
 hapa askari wakiwa wanajadili jambo mara baada ya kutokea ajali hiyo katika maeneo wakiwa na mashuhuda mbalimbali

hapa ni FIRE mara baada ya kufika na kukuta gari likiteketea walianza kuzima moto katika gari hilo kama wanavyoonekana.
NGUDU WANANCHI PANAPOTOKEA MAJANGA YA MOTO MNAOMBWA KUTOA TAARIFA MAPEMA KWA KUPIGA SIMU NO.114 BURE.
tupe maoni yako kama umeguswa na tukio hili, usisahau kulike ukurasa wetu wa facebook

Comments

Popular posts from this blog