Posts

HIKI NDIO CHANZO kuhusu kupigwa risasi kwa mtangazi wa ITV ( Ufoo Saro ) ambaye mama yake naye AMEFARIKI

Image
Alfajiri ya leo, mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua. Akizungumza na mpekuzi wetu, kamanda Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo. Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi. Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili awasuluhishe Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na ndipo alipotoa bast

MASANJA MKANDAMIZAJI AKIWA ANAKULA BATA NDANI YA JIJI LA OBAMA

Image

TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI NA BENKI YA DUNIA ZASAINI MKATABA WA MRADI WA UMEME RUSUMO

Image
  Waziri wa Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa katikati akisaini mkataba wa mradi wa umeme wa Rusumo, kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Burundi Mhe. Tabu Manirakiza, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi Eva Valerian – Washington DC   Naibu Katibu Mkuu, Umoja wa nchi za Afrika Mashariki Dkt. Enock Bukuku akimfafanulia jambo Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula walioko pembeni ni baadhi ya walihudhuria mkutano  wa kusainiwa kwa mkataba wa Rusumo.   Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa akikabidhiwa mkataba na Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce mara baada ya kusaini.   Mawaziri wa  Fedha wa nchi tatu, kutoka  kushoto Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Burudi Mhe. Tabu Manirakiza, Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Wiliam Mgimwa, Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika

Matokeo ya Nani Mtani Jembe kuanza kutangazwa leo

Image
Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akiwakabidhi wafanyakazi wa TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuwashinda wanaoshabikia Yanga katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager inawashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Mariam Martin zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Bahati Msokwa zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nan

Balozi wa Oman amuaga Rais Kikwete

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Oman nchini anayemaliza muda wake Mhe.Yahya Mousa Al Bakary ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Balozi huyo alikwenda ikulu kumuaga Rais(picha na Freddy Maro)   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Oman nchini anayemaliza muda wake Mhe.Yahya Mousa Al Bakary ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Balozi huyo alikwenda ikulu kumuaga Rais(picha na Freddy Maro)

"BREAKING NEWZ"MWANDISHI UFO SARO WA ITV AJERUHIWA KWA RISASI

Image
Habari zilizotufikia zinasema Mwandishi wa habari wa ITV Ufo Saro ambaye anaonekana pichani kulia akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika moja ya kazi zake za kiuandishi amejeruhiwa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo hata hivyo bado taarifa rasmi za chanzo cha tukio hilo hakijafahamika, phars blogspot imeongea kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema bado hawajajua chanzo hivi sasa wanakimbizana kujua hali ya majeruhi na vipi atapa huduma za matibabu ambaye amalazwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, Tunaendelea kufuatilia na kujua taarifa kamili mara tutakapokuwa tayari tutawajulisha kupitia ukurasa huu. TUTAENDELEA KUKUJUZA ZAIDI

Tanzania receives US $ 113.30 from World Bank for Rusumo Falls Hydropower Plant

Image
The World Bank’s Board of Executive Directors today approved US$340 million for the Regional Rusumo Falls Hydroelectric Project which aims to benefit people in Tanzania, Burundi and Rwanda. This project is the first operation under the World Bank Group Great Lakes Regional Initiative inaugurated by the World Bank Group President Jim Yong Kim during his historic joint visit with UN Secretary General Ban Ki-moon in May 2013. The World Bank financing of a total US$340 million – US$113.30 million to the countries of Tanzania, Burundi and Rwanda comes from the International Development Association (IDA). IDA is one of the largest sources of assistance for the world’s 82 poorest countries, 40 of which are in Africa. Resources from IDA bring positive change for 1.8 billion people living on less than $2 a day. Between 2003 and 2013, IDA provided $256 billion in financing for 3,787 projects in Sub-Saharan Africa. IDA established in 1960, helps the world’s poorest countries by providin g

Hermy B kuungana na Jaji Ian na Juliana katika Tusker Project Fame 6, awashauri watanzania kupiga kura

Image
Baada ya kuwafahamu majaji wawili wa TPF6 ambao ni Ian Mbugua (Kenya) na Juliana Kanyomozi (Uganda), hatimaye jina la jaji wa tatu limefahamika ambapo C.E.O wa BHitz Music, Hermes Bariki a.k.a Hermy B (Tanzania) ndiye atakayeungana na majaji hao wawili. Akiongea na 100.5 Times fm Hermy B amewashauri watanzania kuwasapoti washiriki wanne kutoka Tanzania kwa kuwapigia kura kwa kuwa ushindi hutokana na wingi wa kura anazopigiwa mshiriki na sio anachosema jaji. “Watanzania wasifikirie kwamba Jaji wao ndiye atakayewapatia ushindi washiriki wao, ndio wapige kura sasa, kwa sababu ushindi wa watu wengi unatokana na kura na sio jaji, hata Juliana akimwambia you are the best of the best lakini asipopigiwa kura hawezi kushinda.” Amesema Hermy B. Washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika TPF6 ni Angella Karashani a.k.a Angel, Tanah, Hisia na Dubson. Mshindi wa mwaka huu atapewa shilling Million Mia Moja, na mkataba wa kurekodi nyimbo kwa gharama ya shilingi Mil

Habari mbaya: Baba na mama watelekeza watoto wao ndani ya nyumba ....Mama kaolewa kwingine na baba kaoa kwingine

Image
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi mitano bila huduma za msingi. Watoto hao ambao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya. Wakizungumza kwa nyakati tofauti , watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine. Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa nyumba mtaa wa Jakaranda Airport. Watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500 ambazo huzitumia kunun

HOUSIGELI (Mfanyakazi wa ndani ) amnyonga mtoto na kumtupa kwenye dimbwi la maji machafu

Image
Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu. Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake. Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga. AONDOKA NA MTOTO Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza. “Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu. Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwisho

ADAM MCHOMVU "(mtangazaji)awakwaza watu kwa kuweka picha yake mtandaoni akitiririsha KAMASI"

Image
Kupitia Account yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram Mtangazaji wa Clouds Fm Adam amepost picha hii .Ni picha ambayo imezua gumzo sana miongoni mwa mashabiki wake... Wapo wanaohoji UTIMAMU wa akili yake kwa kuweka picha kama hiyo huku wengine wakidai ni bangi zinamsumbua..... Yafuatayo ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake:

KIUNO changu kimeniongezea idadi ya wanaume wanaonitongoza....Wapo wanaotaka kuninunulia gari huku wengine wakiahidi nyumb

Image
Staa wa Majanga, Snura Antony Mushi ‘Snura’ amesema kuwa mauno anayoyakata katika shoo zake yamemfanya apate maombi mengi toka wanaume hasa waume za watu.. Akiongea na mpekuzi wetu, Snura alisema kukata mauno kwenye shoo ndiyo silaha yake ya kuwateka mashabiki lakini anashangaa kuona wanaume za watu ndiyo wanaongoza kwa kumtongoza huku wakiahidi kumnunulia magari na wengine nyumba. “Sipendi kabisa kusikia masuala ya wanaume za watu, Wapo wanaoniahidi gari na wengine nyumba.Labda wangekuwa sio waume za watu ningeweza kufikiria . ,” alisema Snura.

TATOO ya LULU JUU YA MATTITI YAKE YAWA GUMZO

Image
JUZI kabla hajalala mwigizaji Lulu aliwaonyesha mashabiki zake picha ya tatoo yake mpya ambayo imechorwa juu ya Matiti yake kuelekea begani ikiwa ni picha aliyoipost na ikaambatana na maneno yafuatayo:-   "ONLY GOD CAN JUDGE ME…." “ Kumekuwa na kawaida ya watu kuongea na kuhukumu wenzao bila ya kujua wanachokiongelea pengine!! kwa upeo wangu mdogo nafahamu sisi wote ni binadamu na tunamtegemea mtu mmoja MWENYEZI MUNGU… "Lakini cha kushangaza ni kuwa watu wako busy kuhukumu wenzao kuliko hata huyo mwenye cheo chake, hivi Mungu angetaka kufanya kama wanadamu tunavyofanya tungeangaliana kweli? "Nadhani umefika wakati wa kumuachia mwenye majukumu yake kufanya kazi…tuache kujipa u busy usio wa lazma….!!!

Msanii wa Bongo Movie AVULIWA nguo zote na WACHINA na kisha kuchzewa NYETI zake

Image
MSANII wa Bongo Movie, Devota Mbaga hivi karibuni alipatwa na kisanga cha mwaka baada ya kuvuliwa nguo na maofisa wa uhamiaji alipoenda Hong Kong, nchini China kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara. Kwa mujibu wa staa huyo, alifanyiwa kitendo hicho cha kuvuliwa nguo zote na maofisa wa uhamiaji mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na kumsachi kwa kuhofiwa kuwa amebeba ‘unga’. Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Devota alisema baada ya kuvuliwa, alishikwa sehemu zake za siri kitendo alichokiita ni cha kidhalilishaji. “Ilikuwa ni baada ya kugongewa pasipoti yangu nikaingizwa kwenye kitengo cha polisi wa madawa ya kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote ili nikaguliwe,” alisema kwa masikitiko. Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali. Kama vile haitoshi, Devota alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi hilo maofisa hao walimchezea sehemu za kifuani huku wakimwambia kam

NYALLA, NYAULINGO, NYENZI WASHINDA RUFANI

Image
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewarejesha warufani wote watatu katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam. (HM) Samwel Nyalla, Ayubu Nyaulingo na Ayoub Nyenzi walikata rufani mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwaondoa katika uchaguzi huo ambapo wote wanagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali. Akisoma uamuzi wao leo (Oktoba 11 mwaka huu) mbele ya Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF, Jaji Luanda amesema baada ya kusikiliza hoja za Mrufani Nyalla walipitia Kanuni za Uchaguzi za TFF na kugundua yafuatayo; Ibara ya 10(3) imeweka masharti makuu mawili ya ujazaji wa fomu za kugombea uongozi. Fomu hiyo ni lazima iwe na saini ya mgombea na ni lazima ithibitishwe na viongozi wa shirikisho. Kamati imepitia Kanuni za Uchaguzi ha

Kontena zima lakamatwa na MAFUVU na MIFUPA ya binadamu katika bandari ya Mombasa

Image
Wengi walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya binadamu vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya? vinakwenda wapi? kazi yake ni nini? Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii iliyokamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana imesafirishwa na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema ilikua na bidhaa za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu ndipo amri ikatoka kontena likamatwe. Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma Yusuf alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu. Mpaka sasa uchunguzi wa shehena hi