( Miss World 2013 )....Ghana washika nafasi ya tatu Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young wa Philippines baada ya kutwaa taji hilo. Mrembo wa Duinia 2013, Megan Young (katikati) wa Philippines akiwa na mshindi wa pili Marine Lorphelin (kushoto) wa Ufaransa, na mshindi wa tatu Carranzar Naa Okailey Shooter (kulia) kutoka Ghana. Warembo mbalimbali walioshiriki shindano hilo. MREMBO wa Philippines alivishwa taji la binti mzuri zaidi duniani mwaka huu (2013) juzi huko mjini Bali, Indonesia, ambapo kulikuwa na wasiwasi kwamba Waislam wenye msimamo mkali walikuwa wamedhamiria kulivuruga tukio hilo. Mlimbwende huyo, Megan Young, mwenye umri wa miaka 23, aliyezaliwa Marekani, ambaye anachukua mafunzo ya upigaji wa filamu, alipokea taji la mashindano hayo kutoka kwa mshindi wa mwaka jana, Wenxia Yu wa China, na akaahidi kuwa “mlimbwende bora zaidi duniani ambaye hajawahi kutokea". Maelfu ya Waislam wa chama cha Islam Defenders Front waliingia mitaani t