MBINU ZA KUKABILIANA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, KUPIZI HARAKA, NA KUSHINDWA KURUDIA RAUNDI YA PILI
Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume. Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani. Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili. Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi amba