SERIKALI YA MKOA WA RUKWA IKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA KALAMBO YAWATEMBELEA WAHANGA WA AJALI YA BOTI ILIYOUA 13 NA WENGINE 15 KUNUSURIKA KATIKA KIJIJI CHA KIPWA MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA



 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a akitoa baadhi ya maelekezo kwa nahodha wa Boti mara baada ya kuanza safari kuelekea katika Kijiji cha Kipwa mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa ajili ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa ajali mbaya ya kwanza kuwahi kutokea katika Kijiji hicho. Ajali hiyo ya Boti inayodaiwa kusababishwa na hali mbaya ya hewa katika ziwa hilo ilipelekea vifo vya watoto 11 na kinamama wawili. Mtoto mmoja na mama mmoja kati yao ni raia wa nchi jirani ya Zambia na tayari walishapelekwa nchini kwao kwa ajili ya taratibu za maziko. Abiria walookoelewa na kunusurika katika ajali hiyo ni 15 wakiwepo wakinamama 13 na watoto wawili, dereva wa boti hiyo mpaka msafara wa Mkuu wa Wilaya unaondoka kijijini hapo hakufahamika alipo. Abiria hao walikuwa wanatoka katika kijiji cha jirani cha Kapele kufata Zahanati kwa ajili ya chanjo, wakiwa njiani ndio wakapatwa na msiba huo. 

Muongozaji Mkuu wa Blogu ya Rukwareview Hamza Temba hakuwa nyuma kuhakikisha tukio hili zima linaruka hewani, hapo life jacket na kipenga mfukoni chochote kinaweza kutokea; Usalama Kwanza. “…tunashukuru Mungu tulienda salama na kurudi salama…”
Kijiji cha Kipwa kinavyoonekana kutokea ziwani (Tanganyika). Mpasuko wa milima unaoonekana ni kilele cha bonde na mto Kalambo  (Kalambo Falls).
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a akimpa pole Ndugu Hassan Abdul ambaye ni mmoja wa wafiwa katika ajali hiyo mbaya ya boti ilyoua watoto 11 na kinamama wawili. Ofisi ya Wilaya ya Kalambo kwa kushirikiana na Chama Tawala (CCM) ilitoa ubani wa Tsh. 90,000/= kwa kila kaya iliyopatwa na msiba huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a akiwa amemshikilia mtoto Prisila Skapite (7) aliyefanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo kwa kuogelea na kipande cha ubao hadi nchi kavu, mdogo wake aliyemshikilia alifanikiwa kuokolewa pia katika ajali hiyo.
 Mama Roza Zunda naye alifanikiwa kujiokoa na mtoto wake kwa kumshikilia kama inavyoonekana pichani huku akiwa ameshikilia gunia la sabuni lililomsaidia kuogelea hadi nchi kavu na kuookolewa na waokoaji kutoka kijiji cha Kipwa baada ya kuishiwa nguvu.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi wa kijiji cha Kipwa kilichopo mwambao wa Ziwa Tanganyika na kuwapa rambirambi za Serikali ambapo pia aliahidi kurudi katika kijiji hicho kufanya mikutano ya hadhara. Aliahidi kuwa Serikali itasaidia kujenga kituo cha afya katika kijiji hicho pamoja na kufuatilia ujenzi wa barabara itakayosaidia kuunganisha kijiji hicho na maeneo mengine ya Mkoa kutokana na ukweli kwamba kwa sasa kijiji hicho kinafikika kwa njia ya maji peke yake  kwa kutumia Boti.
 Afsa Mkuu wa SUMATRA Mkoa wa Rukwa (kulia) akiwa na DSO Wilaya ya Kalambo wakirudi kutoka katika Kijiji cha Kipwa kwa Boti mara baada ya kutembelea wahanga wa ajali hiyo mbaya ambayo haijawahi kutokea katika kijiji hicho.
Safari ya kurudi
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Comments

Popular posts from this blog