MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria amedhulumiwa viwanja vitatu tofauti mjini Dar es Salaam. Hali hiyo, imesababisha kuwapo na mgogoro mkubwa kati ya familia ya Nyerere na watu ambao wanadai wameuziwa viwanja hivyo miaka kadhaa iliyopita. Viwanja hivyo ambavyo vipo katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kimoja kipo Mikocheni 'B' Plot 402 Block C na kingine kipo Msasani Beach Namba 778, ambacho kinadaiwa kugawanywa kwa watu wawili. Viwanja hivyo, vinadaiwa kuvamiwa na mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, Paul Mushi na mkwe wa Hayati Rashid Kawawa aitwaye Issa Majura Mshangama. Habari za uhakika kutoka ndani ya familia hiyo, zilizothibitishwa kwa MTANZANIA Jumatano na nyaraka mbalimbali, zinasema kutokana na hali hiyo, Mama Maria amelazimika kuiandikia Serikali barua akitaka msaada wa kurudishiwa viwanja vyake. Katika nyaraka hizo, zinaonyesha viwanja hivyo ni mali halali ya mtoto wa tatu wa Mwalimu, John Nyerere. Katika bar