ANGALIA PICHA WATUHUMIWA TISA (9) WA KESI YA WIZI WA MAFUTA KWAKUTUMIA GALI LA KUBEBA WAGONJWA WAFIKISHWA MAHAKAMANI















 MAFUTA YAKIWA NDANI YA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KABLA HALIJAONDOKA


 MAFUTA YAKIWA NJE


 GARI LIKIWA TAYARI KUONDOKA BAADA YA KUPAKIA MAFUTA





 KIJAMPA KIKIWA KIMETULIA








 ENEO HILI LILIKUWA LIMEFICHWA NA PLASTA ILI LISIJULIKANE KUWA NI LA WAGONJWA


 HAPA LIKIWA LIMEFUNIKWA REBO KABLA YA KUGUNDULIKA


 HAWA NDIO WALIOTOA MSAADA WA GARI HILO LA WAGONJWA LILILO GEUZWA KWA WIZI WA MAFUTA





























 HIZI NI PICHA ZA KUTHIBITISHA WIZI HUO WA MAFUTA

Picha na Danice Stephano

 

Na,Denice Stephano




WATUHUMIWA tisa wa kesi ya wizi wa mafuta katika mgodi wa Dhahabu( GEITA GOLD MINE ) kwakutumia gari la wagonjwa (Ambulance) wafikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka matatu yanayowakabili.




Mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Abiner ameiambia mahakama leo (9.9.213) kuwa mnamo 05/09/2013 saa 7:30 usiku uko eneo la Geita power ndani ya mgodi wa geita gold mine watuhumiwa waliiba mafuta lita 630 ya dizeli, kula njama za kuiba mafuta hayo kuaribu mali ambayo ni gari la kubeba wagojwa katika kituo cha Afya cha Nzera kwakuling’oa viti




Mwendesha mashitaka amedai kuwa mtuhumiwa wa kwanza Hamudi Biemo (28) Dereva wa gari hiyo anatuhumiwa na makosa matatu likiwemo la kula njama na kung’oa viti vya gari hilo kwa lengo la kubeba mafuta hayo mwendesha mashitaka huyo ameendelea kuiambia mahakama kuwa watuhumiwa 8 wanakabiliwa na makosa 2 wizi wa mafuta na kula njama ya kuiba mafuta hayo




Abiner ameongeza kuwa washitakiwa hao walitumia gari aina ya Land Crusser yenye namba za usajili T 671 AKW mali ya Halmashauri ya wilaya ya Geita  nakuingia mgodini nakuiba mafuta aina ya Diesel lita 630 zenye thamani ya Tsh. 1,386,000/= mali ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)  




Waliofikishwa mahakamani ni Hamudi Biembo dereva wa gari la wagonjwa ,Malemo Paul (31)  mkazi wa mtaa wa  Mseto Geita,Selemani Magoso (31 )ambaye ni dereva pikipiki mkazi wa mtaa wa Shilabela Geita, Julias Boazi (28) mkazi wa Msalala road Geita )


Wengine ni Rashid Hussen (27) Mlizi wa mgodi, Ismail Zuber (26)mlinzi wa Kampuni ya G4S ,Christoper Kombo Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) Operator wa GGM
 


Naye wakili wa upande wa utetezi Bw. Leonard Bitemo baada ya watuhumiwa kusomewa mashitaka yao nakukana mashitaka hayo wakili huyo aliiomba mahakama ya wilaya kuahirisha kesi hadi wiki tatu  ili wateja wake ambao ni Selemani Magoso, Boaz Paul na ,Milemo Paul wapate nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya utetezi.




Madai hayo yalipingwa na  mwendesha mashtaka  wa poisi na kuomba mahakama ipange  siku za karibu badala ya wiki tatu kwani kuna mashahidi ambao wanasafiri kwenda nje ya nchi, kesi hiyo itajwe 12/09/2013 ambako watakuwa wamejiandaa na mahakama ilikubaliana na uamuzi huo na wasitakiwa wote (9) wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.

Comments

Popular posts from this blog