WAASI CHA FDLR NDIYO KINACHODAIWA KUWA CHANZO CHA KUZOROTA KWA MAHUSIANO MAZURI BAINA YA RAIS JAKAYA KIKWETE NA RAIS POUL KAGAME
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutaba na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda. UHUSIANO tete baina ya Tanzania na Rwanda bado unaendelea kupita chini kwa chini, licha ya viongozi wakuu wa nchi hizo kukutana juzi mjini Kampala, Uganda na kufanya mazungumzo ambayo hayakufika mwisho. Uhusiano huo ulizorota baada ya Rais Jakaya Kikwete kumshauri Rais Paul Kagame, kukutana na waasi wa kikundi cha FDLR kinachopigana mashariki mwa nchi ya Demokrasia ya Kongo (DRC). Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema marais hao walikutana juzi ambapo kila mmoja aliwasilisha dukuduku lake kwa mwenzake. “Walikutana na walipotoka walionyesha nyuso za furaha, kwa kuwa kila mmoja aliwasilisha dukud uku lake. Kila mmoja alieleza j