"Waliopanda mbegu DECI watarudishiwa....."Hii ni kauli ya mahakama
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya sh milioni 21 vigogo wanne wa iliyokuwa Kampuni ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (DECI ). Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Alocye Katemana, pamoja na adhabu hiyo pia ameiagiza serikali ifanye mchanganuo wa mali za DECI ambazo inazishikilia, kwa kuwa zipo mali zilishikiliwa zisizo za kampuni hiyo bali za watu wengine. Alisema kuwa fedha za wateja wa DECI walizopanda zirejeshwe kwa wateja wenyewe ambao wataonesha uthibitisho wa kweli kuwa walipanda fedha zao huko. Katika hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi, Stewart Sanga na kusomwa na Hakimu Katemana, washitakiwa walikuwa watano, ambao ni Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo ole Loitginye, Samwel Mtares na Arbogast Kipilimba. Washitakiwa hao walikuwa wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Hudson Ndusyepo na Onesmo Kyauke. Hakimu Katemana alisema washtakiwa