MAGARI MAWILI YAGONGANA NA TREKTA WATATU WAFARIKI DUNIA
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk. Michael Kadeghe akiwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbozi Ally Wendo katika eneo la ajali leo asubuhi |
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI -AJALI
MNAMO TAREHE 15.08.2013 MAJIRA YA SAA 20:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYABARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.765 BBA AINA YA SCANIA LILILOKUWA
LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUNDUMA LILIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE
BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIGONGA TREKTAAMBALO HALIJAFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI KISHA KULIGONGA GARI ACP 8839 AINA YA SCANIA MALI YA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI YA DHANDHO LILILOKUWA LIKITOKEA TUNDUMA KUELEKEA MBEYA MJINI DEREVA WA GARI HILO BADO KUFAHAMIKA. KATIKA AJALI HIYO WATU WATATU WAWILI KATI YAO WALIKUWA KATIKA GARI T.765 BBA NA MMOJA NI DEREVA WA TREKTA AMBAO HAWAJATAMBULIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO, WOTE WANAUMEWALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO. AIDHA WATU WAWILI WALIOKUWA KATIKA GARI ACP 8839AMBAO PIA HAWAJATAMBULIKA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA WILAYA YA MBOZI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA
WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.
Na Mkwinda Blog
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment