Posts

PROGRAM YA AJIRA KWA VIJANA WALIOHITIMU VYUO VIKUU NCHINI....

Image
PROGRAMU YA AJIRA Programu hii itatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini,Taasisi za fedha na wabia wa maendeleo.Kwa kuanzia utekelezaji wake utaanza kwa kuendeleza programu ya mfano iliyoanzishwa na Idara ya kilimo, uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (DAEA-SUA) na hatimaye kuwafikia wahitimu wa vyuo vingine vya elimu ya juu katika kipindi husika. Kwa kuanzia serikali imekubaliana na Benki ya CRDB kuanza utoaji wa mikopo kwa vijana mara  utekelezaji wa programu utakapoanza. Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya juu nchini imeongezeka wastani wa (48% kwa mwaka) na Wizara imeona vijana wanapomaliza elimu ya juu wanakuwa na elimu ya nadharia katika fani walizozisomea, tumeona kuna umuhimu wa elimu ya ujasiriamli, mitaji na maeneo ya kufanyia uzalishaji na biashara ambavyo ni msingi wa programu hii. Programu hii ni bora kwa kuwa ina vigezo vya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji. MADHUMUNI YA PROGRAMU.

MASAI NYOTAMBOFU AFUNGUKA KUHUSU KITU AMBACHO HATASAHAU, NI ALIVYOTOSWA NA DEMU WAKE KISA HANA PESA

Image
Leo hii bongomovies.com tilifanya interview na mwigizaji wa bongo movies kwa upande wa vichekesho  Gilliady Severine maarufu kama Masai Nyota Mbofu wa Vituko show kwa njia ya simu tokea mkoani Tanga alipo sasa hivi ili tuweze kupata mawili matatu yanayoendelea naye kwa kipindi hiki anachosubiri kufanya video ya wimbo wake mpya na Richie mavoko hivi karibuni. Katika interview hii tulimuuliza mambo mengi sana ila moja ya swali ambalo tulitaka kujua ni jambo gani ambalo hawezi kulisahau tangu alipoingia kwenye sanaa ya uigizaji na muziki. Masai Nyota Mbofu alisema kuwa katika maisha yake anakumbuka sana tukio la kuachwa kwa kejeli na dharau na mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja kisa hakuwa na kitu (Hela) Masai alieleza jinsi ambavyo mrembo huyo aliyemtaja kwa jina moja la Happy la alivyooumiza moyo wake kwa kumdanganya kuwa mtoto (PICHANI) wake huyo aliyezaa naye amefariki dunia ili Masai asie

HAYA NDO MAJIBU YA RAIS MUGABE KWA RAIS OBAMA JUU YA NDOA YA JINSIA MOJA

Image
RAIS WA ZIMBABWE MUGABE KAMCHANA OBAMA,KASEMA HIVIII "Then we have this American president,Obama, born of an African father, who is saying we will not give you aid if you don’t embrace homoséxuality," Mugabe said. "We ask, was he born out of homosexuality? We need continuity in our race, and  that comes from the  woman, and no to  homoséxuality. John and John, no. Maria and Maria, no." ASANTE KWA KUPATA HUDUMA ZETU,TUNAKUOMBA BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOO

MWANAMKE APEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUZINI NA MCHUNGAJI WA KANISA JIJINI DAR

Image
MWANAMKE anayejulikana kwa jina la Nabii Juliana wa Kanisa la Miracle Assemblies of God, amepigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuingilia ndoa ya Mchungaji Richard Kiondo. Tukio hilo la aina yake ambalo lilikusanya umati wa watu, lilitokea hivi karibuni maeneo ya Ukonga Mazizini, jijini Dar ambapo nabii huyo alipigwa hadi kuchaniwa nguo. Akielezea mkasa huo, mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo, Christina Kiondo alisema baba yake alikuwa akishirikiana kwa huduma ya kanisa na Nabii Juliana lakini katika ushirika huo anaamini wawili hao walikuwa na uhusiano usiofaa. Alisema kisa cha nabii huyo kupigwa, hivi karibuni mwanamke mmoja alikwenda nyumbani kwa Mchungaji Kiondo na kuwaeleza watoto hao kwamba anamdai baba yao shilingi 40,000, kitu ambacho kiliwashitua sana kwa kuwa baba yao anaishi kwa nabii na pia hawakujua fedha hizo alikopa kwa ajili ya familia gani. Mtoto mkubwa wa mchungaji huyo, alimtuma mdogo wake nyumbani kwa nabii huyo kwa leng

"NILIJUA TU KWAMBA WANAFIKI WATAFURAHIA MATESO YANGU" ....AGNESS MASONGANGE

Image
VIDEO Queen ambaye hivi karibuni alidaiwa kukamatwa na madawa yanayosadikiwa ni ya kulevya ‘unga’ nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa alijua watu wengi watafurahia kilichompata kwa kumuongelea kila wakati. Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu akiwa Sauzi, Masongange ‘alishauti’ kuwa watu wengi wanamuongelea vibaya bila kujua nini kilichompata  hivyo anaamini hata marafiki zake wa karibu wamefurahia tatizo alilopata. “Najua kabisa kuna watu wengi wamefurahia tatizo nililopata lakini watambue kuwa kila mtu anaweza kupata tatizo hivyo wapunguze kuongea sana bila kujua ni kitu gani kilichotokea juu yangu,” alisema Masogange ambaye atapanda kizimbani kwa mara ya pili mwezi ujao.

KALA JEREMIAH NAYE ATANGAZA NIA YAKE YA KUMPIGIA KAMPENI LOWASSA....ANADAI LOWASSA NI JEMBE

Image
Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini. Usome waraka wake huo wote; Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond. Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa. Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisiasa, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu. Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo una

TASWIRA ZAIDI KUFUNGWA KWA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI MOSHI LEO

Image
Askari polisi waliohitimu mafunzo, wakionyesha pikipiki inavyoweza kusaidia katika kukabiliana na wahalifu kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi mh, dr. emmanuel nchimbi aliyekua mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo ya awali kwa askari polisi na uhamiaji jana mjini moshi. takribani askari polisi elfu tatu na tisini na mbili walihitimu mafunzo, wakiwemo askari wa uhamiaji hamsini na moja. picha na hassan mndeme-jeshi la polisi. Wasanii wa kikundi cha ngoma cha chuo cha polisi Moshi wakitoa burudani jana mjini moshi wakati wa sherehe za kufunga mafunzo ya awali kwa askari polisi na uhamiaji. takribani askari polisi elfu tatu na tisini na mbili walihitimu mafunzo, wakiwemo askari wa uhamiaji hamsini na moja. picha na hassan mndeme-jeshi la polisi. Wahitimu wa mafunzo ya awali ya askari polisi wakifanya onyesho la kareti  jana mjini moshi  wakati wa sherehe za kufunga mafunzo yaliyojumuisha askari polisi na uhamiaji. takribani askari pol

DANGURO LA MAKAHABA LAFUMULIWA

Image
 Hili ni sakata la  kikongwe mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha Makahaba. Mwandishi wetu alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar. Bada ya simu hiyo, uchunguzi wetu  ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa ufuska huo linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee Matutu akidaiwa kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.   Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo hilo,waandishi walivamia eneo la tukio wakiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.   Madanguro hayo ambayo

ANGALIA PICHA ZA WATOTO WALIOZALIWA WAKIWA WAMEUNGANA VICHWA

Image
Watoto mapacha wa k iume wamezaliwa huko India wakiwa na vichwa viwili katika mwili mmoja kitu ambacho inasemekana ni nadra sana kutokea. Madaktari wamesema wanaamini wanauwezo wa kuokoa maisha ya watoto hao ambao wamezaliwa Jumatano (July 24) huko Jaipur, Rajasthan India. Kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mail, nervous system ya watoto hao imetengana wakati uti wa mgon go umeungana na pia wanashare sehemu ya ubavu. Dr. S.D. Sharma, wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni nadra sana kutokea hususan kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama ‘Dicephalic Parapagus’. Aliongeza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea India. Daktari huyo aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye ‘Dicephalic Parapagus’ huzaliwa wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea kwa watoto wa kike. Kwa mujibu wa Sharma alisema kuna uwezekano wa kuokoa maisha ya mapacha hao. Tatizo kama hilo lililowahi kutokea kwa mapacha wa kike kutoka Sudan mwaka (2011) amba

HIZI NDIZO PICHA ZA UGONI ZA NDIKUMANA NA LUCY KOMBA ZINAZOMTESA IRENE UWOYA..!!

Image
LILE sakata la staa wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya kutuhumu kumshika ugoni staa mwenzake aliyemtoa kwenye gemu, Lucy Francis Komba limeingia sura nyingine kuafutia picha za filamu inayodaiwa kuchezwa na wawili hao kunaswa na Ijumaa, twende hatua kwa hatua. Katika baadhi ya matoleo ya Magazeti ya Global Publishers zilichapishwa habari za mastaa hao kuzua bifu zito kufuatia Lucy kumchukua mwanasoka wa Rwanda ambaye ni mume wa ndoa wa Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ na kucheza naye filamu jambo ambalo Uwoya alilipinga. KWA NINI UWOYA ALIPINGA? Uwoya alipinga mumewe kushiriki filamu hiyo kwa sababu aliambiwa washiriki ni wawili tu, mumewe Ndikumana na Lucy. Filamu inaitwa Kwa nini Nisimuoe? Kwa mujibu wa Uwoya, hajawahi kuona filamu ya kawaida inachezwa na watu wawili tu, akasema Lucy alitumia nafasi hiyo kuwa na mumewe kimapenzi. Hata hivyo, Uwoya alisema akiviona vipande vya picha za filamu hiyo atajua ukweli. Wiki iliyopita aliviona vipande hi

HUYU NDO MSANII ALIYETANGAZA KUMPORA MUME WA AUNT EZEKIEL...

Image
KATIKA hali isiyo ya kawaida msanii anayechipukia katika filamu za Kibongo, Isabella Fransis ‘Vai wa Ukweli’ anamtafuta ubaya gwiji katika tasnia hiyo, Aunt Ezekiel kwa kusema anamtamani mumewe. Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt. Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.  “Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai. Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini kuwa anafaidi sana kwa kuwa na mwanaume huyo.   Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya.  

POLISI 3,092 WAMEHITIMU MAFUNZO CCP MOSHI WANAKUJA MTAANI

Image
 Zaidi ya Askari Polisi wapya 3,092 wamehitimu mafunzo yao ya awali ya Polisi katika Chuo cha Polisi (CCP) kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro hii leo. Polisi hao wapya ambao wanaingia mtaani nchi nzima wataingia mtaani wakati wowote kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao unakuwa madhubuti. Mafunzo yao yamefungwa chuoni hapo na Waziri Mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa kushuhudia maonesho mbalimbali ya vitu walivyo jifunza jambo ambalo endapo kama watalitumia vyema basi litaleta chachu katika kukabiliana na uhalifu unao tikisa katika maeneo mbalimbali ya nchi pamoja na watu wasio tii sharia hadi washurutishwe. NA FATHER KIDEVU  Maonesho ya Careti yakifanyika  Kareti hiyoo Ukakamavu

IRENE UWOYA AREJEA NCHINI AKITOKEA SWAZILAND....ADAI KUPEWA SHAVU LA NGUVU NA KING MUSWAT.

Image
  Mwigizaji Irene Uwoya amerejea nchini toka nchini Swaziland alipokuwa kwa takribani wiki tatu.   Irene Uwoya aliyerejea nchini leo hii amerejea na salamu toka nchini Swaziland alizoziandika kupitia ukrasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii alisema…   “Mswat anawasalinmu sana! Nahiv karibun atatinga hapa nakanipa kibali chakufanyya move na ful suport...I wl prove u wrong...try me”   Akimaanisha, amerejea nchini na Mswati amnawasalimia sana na amesema atakuja nchini hivi karibuni na amenipa kibali cha kufanya Filamu na atanisaidia kwa kila kitu. Nijaribu nitakuthibitishia kuwa umekosea ( Kwa Kiswahili fasaha ).   Bado tunamtafuta Irene amabaye namba yake ya simu haipatikani kujua kama kauli hii ni ya kweli au anawatania tuu mashabiki wake.

Vicent Kigosi (Ray) Atoa mtazamo wake kuhusu maisha na hiki ndicho alicho kisema Soma zaidi

Image
Leo tunawaletea mkusanyiko wa mambo kumi toka kwa  mwigizaji mkongwe nchini Vicent Kigosi (Ray) kuhusu maisha na namna ambayo anafikiri kuhusu maisha ya kila siku ya mwanadamu. Maoni haya tumeweza kuyapata  baada ya kufanya uchambuzi yakinifu kwenye akaunti mbalilmbali za mwigizaji huyu za kwenye miandao ya kijamii na kuzipanga kwa jinsi ambavyo tunaona stahili. Soma hapo chini ujue mwigizaji huyu huwa anawaza nini kuhusu maisha.     Mungu ndio kila kitu katika dunia hii     Amani ndio kitu cha msingi kwenye nchi yetu ya Tanzania     Mungu ni mwema sana katika maisha ya binadamu     Ukiwa na uwezo wa pesa ishi na watu vizuri     Pambana kijana na maisha wakati wako ndio huu     Hakuna kitu muhimu duniani kama kuwekeza kwa jamii     Mazoezi ni bora kwa afya yako     Pole pole ndio mwendo ukiwa na haraka waweza kujikwaa     Kama unapata kumi kwanini usipate na mia?     Mwisho wa ubaya ni aibu

HAKUNA AJALI YA TRENI KAMA HII ILIYOWAHITOKEA SPAIN

Image
Treni iendayo mwendo kasi imepata ajali huko northwestern Hispania ambapo inaaminika watu 20 wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa kati ya abiria 200 waliokua wakisafiri nayo. Moja ya mabehewa limeonekana likiwa linawaka moto na jingine kukatika katikati kwenye eneo la ajali hiyo karibu na Santiago De Compostela ambapo ilikua ikisafiri kuelekea Ferrol Northwest Spain.

HIVI WATANZANIA TUMEKOSA UTU KIASI HICHI?

Image
Watanzania wenzetu wanavua samaki kwa kutumia sumu, wengine wanakaanga chips kwa mafuta ya transformer, kuku wanakuzwa kwa contraceptives (dawa za uzazi wa mpango), kitimoto nao wanapewa ARV's, samaki wanahifadhiwa kwa formalin (dawa ya kuhifadhia maiti) si hivyo tu, dawa feki kila kona? Vyote hivi in a long run vitawaathiri watanzania wengi! Tunauana wenyewe kwa wenyewe kwa tamaa ya kutajirika haraka haraka! Mimi huu ujinga unanikera sana! !

MAREKANI YAMPA ONYO RAIS KAGAME WA RWANDA....YAMTAKA KUACHA MARA MOJA KUWASAIDIA WAASI WA M23

Image
Marekani imeitaka Rwanda kuacha kusaidia waasi wa kundi la M23 ambalo linaendesha mapambano dhidi ya Serikali ya nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Taifa hilo kubwa duniani limesema lina ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa Rwanda inalisaidia kijeshi kundi hilo la waasi na baadhi ya maofisa wake wamo. Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kutoa kauli kali tangu kundi hilo lianzishe mapigano dhidi ya Serikali ya DRC katika mji wa Goma ulioko eneo la Mashariki, ambalo lina utajiri mkubwa wa madini. "Tunaitaka Rwanda iache mara moja kutoa msaada wa aina yoyote kwa M23," alisema Jen Psaki, Msemaji wa Ikulu ya Marekani. Msemaji huyo pia aliitaka Rwanda iondoe wataalamu wake wa kijeshi ndani ya M23. Marekani imetoa agizo hilo zikiwa zimebaki siku mbili kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje, John Kerry kuongoza kikao maalumu cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) ambacho kitajadili masuala ya Afrika hasa amani ya eneo la Maziwa Makuu. Kundi la