MASAI NYOTAMBOFU AFUNGUKA KUHUSU KITU AMBACHO HATASAHAU, NI ALIVYOTOSWA NA DEMU WAKE KISA HANA PESA



Leo hii bongomovies.com tilifanya interview na mwigizaji wa

bongo movies kwa upande wa vichekesho  Gilliady Severine maarufu
kama
wa Vituko show kwa njia ya simu tokea mkoani Tanga alipo sasa hivi ili
tuweze kupata mawili matatu yanayoendelea naye kwa kipindi hiki
anachosubiri kufanya video ya wimbo wake mpya na Richie mavoko hivi
karibuni.




Katika interview hii tulimuuliza mambo mengi sana ila moja ya

swali ambalo tulitaka kujua ni jambo gani ambalo hawezi kulisahau tangu
alipoingia kwenye sanaa ya uigizaji na muziki.





Masai Nyota Mbofu alisema kuwa katika maisha yake anakumbuka

sana tukio la kuachwa kwa kejeli na dharau na mpenzi wake aliyezaa naye
mtoto mmoja kisa hakuwa na kitu (Hela)



Masai alieleza jinsi ambavyo mrembo huyo aliyemtaja kwa jina

moja la Happy la alivyooumiza moyo wake kwa kumdanganya kuwa mtoto
(PICHANI) wake huyo aliyezaa naye amefariki dunia ili Masai asiendelee
kumsumbua na mpenzi wake huyo mpya.



Akiongea kwa huzuni masai amesema akikumbuka huwa anaumia sana

kwani alitoka mbali sana a binti huyo na haelewi kwanini aliamua
kumfanyia hivyo kisa kapata mpenzi mpya badala ya kumwambia ukweli tuu
kwani alikaa kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja akijua motto wake
kafariki kabla ya kuja kugundua kuwa yupo hai na mzima wa afya.



Masai kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya video yake

mpya ya muziki unaoitwa "Yero
Masai" aliyofanya na Richie Mavoko na kitokolo video
itayofanywa na Apex Videos chini ya director Pablo.


Comments

Popular posts from this blog