PROGRAM YA AJIRA KWA VIJANA WALIOHITIMU VYUO VIKUU NCHINI....
PROGRAMU YA AJIRA Programu hii itatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini,Taasisi za fedha na wabia wa maendeleo.Kwa kuanzia utekelezaji wake utaanza kwa kuendeleza programu ya mfano iliyoanzishwa na Idara ya kilimo, uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (DAEA-SUA) na hatimaye kuwafikia wahitimu wa vyuo vingine vya elimu ya juu katika kipindi husika. Kwa kuanzia serikali imekubaliana na Benki ya CRDB kuanza utoaji wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa programu utakapoanza. Kwa kuwa kasi ya wanaojiunga elimu ya juu nchini imeongezeka wastani wa (48% kwa mwaka) na Wizara imeona vijana wanapomaliza elimu ya juu wanakuwa na elimu ya nadharia katika fani walizozisomea, tumeona kuna umuhimu wa elimu ya ujasiriamli, mitaji na maeneo ya kufanyia uzalishaji na biashara ambavyo ni msingi wa programu hii. Programu hii ni bora kwa kuwa ina vigezo vya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji. MADHUMUNI YA PROGRAMU.