Posts

Msafara wa Baba Mtakatifu Francis 1 wapotea njia nchini Brazil ukitokea uwanja wa ndege.

Image
  Maelfu ya wananchi wa Brazil katika mitaa ya Rio de Janeiro wameivamia na kulizunguka gari lilokuwa limembeba  Baba Mtakatifu Francis 1 wakati msafara wake ulipopotea njia ulipokuwa ukitokea uwanja wa ndege alipowasili nchini humo kwa ziara. Katibu wa Usafiri wa Rio Carlos Osorio amesema gari aina ya Fiat alilokuwemo Baba Mtakatifu lilikuwa likitokea uwanja wa ndege kuelekea katikati ya mji, lilipita njia tofauti lilipofika katika mgawanyiko wa barabara 12 unaofahamika kama Avenida Presidente Vargas. Badala ya kupita njia za upande wa kushoto za mgawanyiko huo ambako hakukuwa na msongamano wa magari, gari hilo lilipita njia za upande wa kulia ambako kuna magari mengi yakiwemo mabasi na teksi nyingi, hatua iliyosababisha gari hilo kusimama. Maelfu ya watu waliokuwa wamejipanga mitaani walilikimbilia gari hilo na kufika katika dirisha la upande alipokaa , huku wengi wao wakimpiga picha. Msemaji wa Vatican Padri Federico Lombardi amet

Bomu lanaswa ziara ya Papa Francis nchini Brazil

Image
  Mbali ya kufurahia mapokezi makubwa nchini Brazil, ziara ya Papa Francis imeingia doa baada ya bomu kugunduliwa chooni katika mji ambao atauzuru leo. Bomu hilo la kutengenezwa kienyeji liligunduliwa na maofisa usalama likiwa katika choo katika Kanisa la Bikira Maria wa Aparecida katika mji huo mdogo ambao kiongozi huyo atautembelea kama sehemu ya ziara yake kwa kwanza nje ya Vatican. “Lilikuwa bomu la kutengenezwa kienyeji lenye uwezekano mdogo wa kusababisha maafa,” imeeleza taarifa ya Jeshi la Anga la Brazil. “Ni tukio linaloshtua, limefanyiwa kazi na wana usalama ambao wamejiandaa vyema kwa ziara hii. Kwa hakika haliwezi kuzua hofu, vikosi vya usalama vimejiandaa kikamilifu kwa matukio kama haya.” Kulingana na vyombo hivyo, bomu hilo liliteguliwa na kisha kuharibiwa baada ya kugundulika kwake katika mji huo mdogo kwenye viunga vya Rio de Janeiro baada ya mazoezi ya vikosi vya usalama, limeeleza gazeti la Grupo Estado. Bikira Maria wa Aparecid

POLISI 117 WATIMULIWA KAMBINI KWA UTOVU WA NIDHAMU

Image
Wanafunzi 117 wa Polisi, wamefukuzwa katika Chuo cha Taaluma na Mafunzo ya Polisi (MPA), kilichopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.  Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya. Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni mkuu wa chuo hicho alisema katika mahojiano maalumu kwamba, waliotimuliwa chuoni ni kati ya askari wanafunzi 3,189 waliokuwa wamesajiliwa kuanza mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho, Oktoba 25 mwaka jana.   Kati yao askari 115 ni wale wa Polisi na askari wawili wanatoka katika Idara ya Uhamiaji iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kufukuzwa kwa wanafunzi hao , kuna akisi moja kwa moja jinsi menejimenti ya chuo hicho ilivyojipanga upya kupunguza wimbi la baadhi ya askari walioko kazini na ambao wanalipaka matope jeshi hilo kutokana na kupotoka kimaadili kwa kutaka kujinufaisha k

HUYU NDIE MTANZANIA MWENYE WATOTO KUMI SOMA NA SHUHUDIA MWENYEWE

Image
Bi. Rejina Moshwa (37) mkazi wa Kijiji cha Isoso akizungumza na mwandishi wa habari kutoka Clouds FM Aziz Kindamba Paschal Kulwa Manyinzi (42) mkazi wa Kijiji cha Isoso akiwa katika picha na baadhi ya watoto wake baada ya mazungumzo na Thehabari.com ……………….. Na Thehabari.com, Kishapu WASUKUMA ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo awali yalishikilia desturi ya familia kuwa na idadi kubwa ya watoto. Familia moja yaani baba na mama waliendelea kuzaa kadri walivyo jaaliwa kupata watoto bila kujali ukubwa wa familia. Mume pia hakuwa na kizuizi katika familia cha kuongeza mke mwingine endapo atakuwa na ardhi (mashamba) na mifugo (hasa ng’ombe) ya kutosha kuweza kuihudumia familia aliyonayo. Wapo walioamini kwamba kuwa na ukubwa wa familia ni kuongeza nguvu kazi katika uzalishaji kwa kutumia ukubwa wa familia. Hata hivyo pia wapo walioamini uzazi ni mpangilio wa Mungu hivyo haupaswi kupangiliwa na wazazi bali mola mwenyewe.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI, CHANGAMOTO ZA MAENDELEO NA UKUAJI WA MIJI BARANI AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi  wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji Barani Afrika.  Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini Arusha. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi , kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi ‘Physical Sciences’ (COSTECH) Prof. Clavery Tungaraza,  baada ya Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013.  Picha na OMR Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya  ufunguzi. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mo

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA MAMA CHERRIE BLAIR NA AFUTURISHA VIONGOZI NA WANAKIJIJI CHA HOYOYO. IMG_7126

Image
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Cherrie Blair wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, mara baada ya kufanya mazungumzo yao. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mama Cherrie Blair, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza walipokutana kwenye ofisi za WAMA tarehe 23.7.2013 Mama Blair yupo nchini akifuatana na mumewe Tonny Blair katika ziara ya kikazi. ke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake baada kuwafuturisha viongozi wa serikali, madhehebu ya dini wa wilaya ya Mkuranga na wananchi wa kijiji cha Hoyoyo kilichoko karibu na Mkuranga katika Mkoa wa Pwani tarehe 23.7.2013.  NA FULLSHANGWE BLOG ke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake baada kuwafuturisha viongozi wa serikali, madhehebu ya dini wa wilaya ya Mkuranga na wananchi wa kijiji cha Hoyoyo kilichoko karibu na Mkuranga katika Mkoa wa Pwan

IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA WASHIKANA UGONI

Image
NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake. “Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema  ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira. Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy.   “Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu

KAHABA LANASWA LIKIFANYA NGONO KATIKA MAKABURI YA MALAPA BUGURUNI

Image
LICHA ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watu wengi kuogopa kufanya maovu, jimama anayekwenda kwa jina la Joyce Benson (34), amefumwa akifanya ngono katika makaburi ya Malapa, Buguruni jijini Dar. Joyce amekamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita saa nane katika maeneo hayo akifanya biashara haramu ya kuuza mwili wake katika makaburi hayo kwa njia ya kujipatia fedha.   Joyce mwenye umbile la miraba minne alipatwa na fedheha kubwa baada ya majirani zake kusikia habari hizo na kuanza kumlaani. Mbali na Joyce pia siku hiyo machangudoa wengine 14, waliokuwa wakifanyia vitendo vya ukahaba kwenye makaburi hayo walikamatwa. Joyce na wenzake hao walifikishwa katika Mahakama ya Jiji (Sokoine Drive) ili sheria ifuate mkondo wake. Wakiwa mahakamani hapo, mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi aliwasomea tuhuma za kufanya ukahaba na kumfanya hakimu wa mahakama hiyo, Timoth Lyon kupigwa na butwaa. Hata hivyo, Joyce na wenzake walikana kufanya kosa hilo ambapo

RAIS KIKWETE AINGILIA KATI KODI ZA LINE.....

Image
HATMAYE RAIS KIKWETE AMEZITAKA MAMLAKA HUSIKA ZIKUTANE HARAKA ILI TATIZO LIISHE Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi. Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika

VAZI LA NUSU UCHI LAZUIA NDOA KUFUNGWA JIJINI DAR....PADRI AGEUKA MBOGO NA KUWATIMUA WAPAMBE

Image
KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae vizuri. “Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,” alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam. Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani. Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha. Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimis

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar lakamata silaha 7 na majambazi 8 na pia lakanusha Mh. Mnyika kukoswa na bomu.

Image
  Baadhi ya askari polisi wakionyesha kwa waandishi wa habari silaha zilizokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa matukio ya ujambazi. DCP Mlege akitoa taarifa ya mafanikio ya Jeshi hilo kwa waandishi wa habari ambapo akizungumzia suala la Mh. Mnyika amesema askari No. E. 5340 D/CPL Julius aliyekuwa ndani ya gari la polisi PT. 1902 alikuwa anasogeza boksi lenye mabomu ya kutoa machozi ya kurusha kwa mkono, kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo na halikuleta madhara yeyote kwa askari polisi wala raia waliokuwa eneo la uwanja wa Sahara uliopo Mabibo ambako chama cha CHADEMA kilikuwa kifanye mkutano wa hadhara tarehe 21 Jula 2013 kinyume na utaratibu. Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata sila 5 ikiwemo SMG moja, Shortgun mbili, Riffle Mark 3 tatu, Pisto moja, Risasi 56, Maganda ya Risasi 17 na Majambazi 8. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba