BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LAAPISHWA MISRI
Rais wa mpito wa Misri ameliapisha baraza lake jipya la mawaziri huku akiwapa nafasi viongozi wenye msimamo wa kati na pia akiwajumuisha wanawake wawili kwenye Serikali mpya. Serikali mpya inaongozwa na waziri mkuu, Hazem el-Beblawi ambaye kwa taaluma ni mchumi, Abdel-Fattah al-Asisi ambaye ataendelea kushikilia nafasi yake ya waziri wa ulinzi na pia Kama naibu waziri mkuu wa kwanza. Waziri wa masuala ya ndani ambaye aliteuliwa na rais aliyepinduliwa, Mohamed Ibrahim ataendelea kushikilia wadhifa wake, huku Nabil Fahmy ambaye aliwahi kuwa balozi wa Misri nchin Marekani, sasa atakuwa Kama waziri wa mambo ya nje. Akisisitiza kwanini baraza lake limejumuisha viongozi wenye msimamo wa Kati, rais wa mpito, Adly Mansour amesema amazingatia mahitaji ya nchi huku akitangaza nafasi tatu za wanawake kwenye baraza lake. Wizara walizopewa wanawake hao ni pamoja na wizara ya habari, wizara ya afya na wizara ya mazingira, uteuzi ambao unaonekana haukutar...