Posts
ANGALIA PICHA KIJANA "ANG'OLEWA" MENO 232
- Get link
- Other Apps
Madaktari nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba. Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye t aya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai. Kijana huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo cha tatizo. Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia". Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili. Ashik sasa ana meno 28. "Ashik aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware. "Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazi
AJALI NYINGINE YA NDEGE YAUA ZAIDI YA 40
- Get link
- Other Apps
Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne. ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu. Meneja Mkuu wa TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio. Siku za hivi karibuni Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua. Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati visanduku
MBASHA AKANA KUMBAKA SHEMEJI YAKE
- Get link
- Other Apps
KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa. Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani. Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti. Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli. Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa kati
DIAMOND ATAJWA KUWANIA TUZO ZA TFAAS,KUCHUANA NA YAYA TOURE
- Get link
- Other Apps
Diamond Platinumz anaendelea kuongeza CV katika muziki wake kwenye level za kimataifa baada ya kutajwa Jana kuwa mmoja kati ya vijana wa Afrika wanaowania tuzo kubwa ya The Future Africa Awards& Summit (TFAAS 2014) zitakazofanyika Lagos Nigeria, July 31. Waandaaji wa tuzo hizo wametangaza vipengele kumi vyenye majina matano katika kila kipengele baada ya kupokea mapendekezo kutoka katika bara zima la Afrika kupitia kamati yake maalum. Utoaji wa tuzo hizi unatajwa kuwa tukio la pili kwa ukubwa linalohusu vijana kaika bara la Afrika. Diamond anawania kipengele cha The Future Africa Awards Prize in Entertainment akiwa na Ice Prince, Yaya Toure (Iviry Coast), Sarkodie (Ghana) na muigizaji Ivie Okujaye (Nigeria). Washindi wa tuzo hizi watapatikana kupitia jopo maalum lilotajwa na kamati ya tuzo hizo. Katja Schiller Nwator (Leadership Development and CSR Manager, The Tony Elumelu Foundation), Mahamadou Sy (Founder and Executive Director of the Institut
MTOTO WA MIAKA 12 AFUNGUKA ALIVYOFUNDISHWA UCHAWI
- Get link
- Other Apps
Mtoto (kulia jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 anayemtuhumu baba yake kumfundisha uchawi. MTOTO mmoja mkazi wa Kimara Salanga, jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 hivi karibuni aliibuka na kutoa madai mazito, akimtuhumu baba yake mkubwa kuwa alimfundisha uchawi, Ijumaa lina mkasa kamili. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mtoto huyo alisema alianza kufundishwa tabia hiyo mbaya na baba yake mkubwa wakati huo akiwa na umri wa miaka mitano jijini Mbeya, kwa kumwelekeza namna ya kuroga na kuua watu. Katika mojawapo ya matukio makubwa aliyodai kuwahi kuyafanya ni pamoja na kutengeneza ajali ya boti iliyotokea Nungwi mapema mwaka huu ambapo yeye na wenzake walitumwa na baba yake huyo kutega mambo yao huku wengine wakipanda kwenye chombo hicho ili kuongeza uzito uliosababisha boti hiyo kuzama na kuua watu kibao. “Tuligandisha maji na kuweka sindano ambazo zilitoboa na baada ya watu kufa tulichukua nyama na damu