ANGALIA PICHA KIJANA "ANG'OLEWA" MENO 232
Madaktari
nchini India wametoa meno 232 kutoka katika mdomo wa kijana mwenye umri
wa miaka 17, katika upasuaji uliochukua saa saba.
Kijana huyo Ashik Gavai alifikishwa hospitali akiwa amevimba na maumivu kwenye taya na shavu lake la upande wa kulia, amesema Dokta Sunada Dhiware, mkuu wa idara ya meno katika hospitali ya JJ jijini Mumbai.
Kijana
huyo amekuwa akisumbuliwa kwa miezi 18, na alilazimika kusafiri kwenda
mjini, baada ya madaktari katika kijiji chake kushindwa kufahamu chanzo
cha tatizo.
Madaktari wameelezea hali hiyo kuwa "ni haba sana" kutokea na ni jambo ambalo "limevunja rekodi ya dunia".
Upasuaji huo uliofanyika siku ya Jumatatu, ulihusisha madaktari wawili na wasaidizi wawili.
Ashik sasa ana meno 28.
"Ashik aligunduliwa kuwa na
ugonjwa wa aina yake ambao ufizi mmoja huunda meno mengi. Ni kama aina
ya uvimbe wa saratani," amesema Dokta Dhiware.
"Mwanzoni, hatukuweza kukata fizi, kwa hiyo tulilazimika kutumia nyundo na tindo kufanikisha.
"Tulivyopasua tu, meno madogo
madogo yakaanza kutoka, moja baada ya jingine, na tulipoyahesabu,
yalifika meno 232." Amesema daktari huyo.
Comments
Post a Comment