MTOTO WA MIAKA 12 AFUNGUKA ALIVYOFUNDISHWA UCHAWI

 Mtoto (kulia jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 anayemtuhumu baba yake kumfundisha uchawi.
MTOTO mmoja mkazi wa Kimara Salanga, jijini Dar es Salaam (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 12 hivi karibuni aliibuka na kutoa madai mazito, akimtuhumu baba yake mkubwa kuwa alimfundisha uchawi, Ijumaa lina mkasa kamili.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, mtoto huyo alisema alianza kufundishwa tabia hiyo mbaya na baba yake mkubwa wakati huo akiwa na umri wa miaka mitano jijini Mbeya, kwa kumwelekeza namna ya kuroga na kuua watu. 

Katika mojawapo ya matukio makubwa aliyodai kuwahi kuyafanya ni pamoja na kutengeneza ajali ya boti iliyotokea Nungwi mapema mwaka huu ambapo yeye na wenzake walitumwa na baba yake huyo kutega mambo yao huku wengine wakipanda kwenye chombo hicho ili kuongeza uzito uliosababisha boti hiyo kuzama na kuua watu kibao. 
“Tuligandisha maji na kuweka sindano ambazo zilitoboa na baada ya watu kufa tulichukua nyama na damu kwa ajili ya kula na kunywa. Kwa hiyo nimeua na kula nyama za watu.
Baadhi ya tunguli za uchawi zilizokuwa zikitumiwa na mtoto huyo.
 “Pia niliwahi kutumwa kwa msichana ambaye nilimnyunyizia dawa, nikamkalia na kumkaba shingoni mpaka akafa, nikamchukua na kumpeleka kwa baba mkubwa, pale kitandani niliacha gogo ambalo lina sura yake, kule tulimla na kunywa damu yake sisi na wachawi wenzetu. 
“Baada ya kufanya matukio hayo mazito, baadhi ya wananchi waliponigundua kuwa ni mchawi, walienda kunishtaki kwa mama yangu mzazi, wakimwambia asiponihamisha wataniua. 
“Kwa hali hiyo, huyu mjomba wangu akanileta Dar kwa ajili ya kufanyiwa maombi, lakini siku ya kwanza tu baada ya kufika, wakati nakwenda kuchota maji nilikutana na mmoja (jina limehifadhiwa) aliyeniambia kumbe mimi ni kijana wa kazi, alinitambua kutokana na nyota tunayobandikwa kwenye paji la uso baada ya kujiunga na uchawi ambayo ukikutana na mwenzako mnatambuana.“Baada ya kuniambia hivyo, usiku wake nikiwa nimelala, baba mkubwa alikuja kichawi na kunichukuwa na kunipeleka kwa yule mzee ambaye ndiye mkuu wa wachawi wa eneo hili, akanikabidhi kwake na mikoba yangu ya kichawi na hapo ndipo nikaendelea na kazi kwa upande wa huku Dar nikishirikiana na wachawi wengine.
“Kazi yetu mara nyingi ni kuloga, kuua na kunyunyizia dawa kwenye makaburi, yakifunguka tunachukuwa nyama za watu na mafuvu na kuyapeleka nyumbani kwa yule mkuu wa wachawi wa eneo hili tunapokutania. 
“Hapa nyumbani kwa mjomba niliweka dawa kwenye ukingo wa nyumba ili wasimalizie kujenga na kumloga mkewe ambaye tulimtupia vidonda vya tumbo, nilitaka kumuua lakini maombi yalimsaidia,” anasimulia kijana huyo. 
ATINGISHA KIJIJI CHA SALANGA
Kwa mujibu wa shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Lucy, baada ya kufanyiwa maombi kanisani kwa Mwingira, mtoto huyo alikiri kuachana na uchawi lakini alikuja kugundua bado anaendelea kutokana na kufanya maombi ya kufunga ambapo aliona katika maono kuna dawa ameweka kwenye nguo zake alizokuwa akipenda kuzivaa kila siku. Alipobanwa kwa vitisho ndipo aliwataja wachawi wenzake na kuongeza kuwa kila alipokuwa akitoka kwenye maombi, anakutana na wachawi wanamvisha uchawi tena na ule wa tumboni aliolishwa bado unaendelea kufanya kazi. 
WATINGA KWA MJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA
Baada ya kueleza mambo hayo mazito waliamua kutinga kwa mjumbe ambaye baada ya kuwasikiliza aliitisha kikao cha pamoja na yule mzee ambapo mtoto huyo alieleza kinagaubaga mbele ya wananchi mambo wanayofanya wakiwa na mzee huyo lakini alikataa na kuapa kwa kutumia msahafu kuwa anasingiziwa na kwamba hajawahi kufanya mambo hayo. 
NYUMBANI KWA MZEE ANAYEDAIWA MCHAWI
Mapaparazi wetu walitinga nyumbani kwa mzee huyo ili azungumzie suala hilo lakini jitihada ziligonga mwamba baada ya kumkosa ambapo mkewe anayedaiwa  kushirikiana naye kwenye mambo hayo, aliyejitambulisha kama mama Isha, alisema; “Ni kweli huyo mtoto alieleza mambo hayo kwa mjumbe lakini naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mimi na mume wangu siyo wachawi, hayo ni maneno ya uzushi tu, watu wa kijiji hiki wanatuonea wivu kwa sababu tuna maendeleo kwani hawapendi mtu awe na mafanikio,” alisema.

Comments

Popular posts from this blog