ATCL Yaondolewa International Air Transport Association kwa Madeni
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limeondolewa katika Mfumo wa Malipo wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (International Air Transport Association – IATA) kutokana na kukabiliwa na madeni na sasa iimetiliana saini ya makubaliano ya miaka mitano na Kampuni ya Ndege ya HAHN Air ili kuuza tiketi za Air Tanzania.
Akizungumza na wanahabari Mjini Zanzibar, Mkurugenzi wa ATCL. Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi, amesema wamelazimika kuingia kwenye makubalianao na kampuni hiyo ili wasikose baadhi ya huduma za malipo ya tiketi.
“Tuna madeni, sikumbuki yalifikia kiasi gani lakini ni madeni makubwa ambayo yalilazimisha kusimamishwa uanachama au kufungiwa huduma hizi mpaka tutakapokuwa tumelipa hayo madeni.
“Kubwa zaidi ilikuwa ni sisi kuwa katika mfumo wa Shirikisho wa Mashirika ya Ndege Dunia IATA ambayo ndiyo mfumo wa uuzaji na utawanyaji wa tiketi kwa kuwa mabadilishano ya pesa au kupeleka pesa kutoka shirika moja kwenda lingine hufanyika kwa kutumia huo mfumo wa IATA. Hii tunaanza kufanya kwa kweli ni kupitia k mgongoni kwa mtu.
“Hawa ni wanachama ambao wamepewa leseni ya kutoa huduma kwa mashirika ambayo hayapo kwenye mfumo wa IATA. Lazima tulipe madeni yetu tuliyonayo IATA ambayo ni mabilioni ya pesa ili tuweze kurudi kwenye mfumo wa kukusanya pesa,” alisema Mhandisi Matindi.
Comments
Post a Comment