Posts

MWAKILISHI WA SHIRIKA LA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA (UNDP) ATEMBELEA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Image
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimkabidhi Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015, Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson, wakati kiongozi huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto katikati) akimueleza jambo mgeni wake ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.  Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume y

Waendesha Bajaji Wenye Ulemavu Wafunga Barabara Dar

Image
Dar es Salaam: Waendesha Bajaji wenye ulemavu wanaofanya shughuli zao katika Jiji la Dar es Salaam wamelazimika kufunga barabara ya Mission na kuzuia magari kuingia katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala. Wamefanya hivyo kwa lengo la kushinikiza wapewe vituo maalum vya kupakia na kushusha Abiria katikati ya jiji. Tupia Comm

Picha: Thomas Mashali Alivyozikwa Jijini Dar Leo

Image
Hatimaye mwili wa bondia Thomas Mashali umezikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar mchana huu. Picha zote na Boniphace Ngumije / GPL

MBUNGE Godbless Lema ALETA HALI TETE BUNGENI…Adai Waziri Alimshauri Wafanye Fujo Arusha ili Aingilie

Image
GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini amesema kwamba, alishauriwa na George Simbachawene, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa, amfungie ofisini Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ili kuibua vurugu na kisha (Simbachawene) aingilie, anaandika Charles William.Akizungumza bungeni leo asubuhi, Lema amesema Simbachawene alimtaka yeye na viongozi wengine wa Chadema wamfanyie vurugu mkurugenzi huyo kisha tukio hilo lioneshwe katika Runinga ili waziri aingilie kati mgogoro huo kwa madai, utakuwa umedhihirika. “Nilimwambia Waziri Simbachawene kuwa Arusha tuna tatizo kwenye halmashauri tunaomba msaada, akanishauri tukafanye fujo ili aone kwenye vyombo vya habari na apate nafasi ya kuingilia mgogoro huo kwasababu rais amewapa nguvu wakuu wa mikoa. “Akaniambia siwezi kuja kichwa kichwa nenda kafanye fujo, mfungieni mkurugenzi nje halafu mimi nione kwenye TV ili niingilie mgogoro huo. Yaani waziri anaogopa kuingilia migogoro

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA TUKIO LA MOTO, BANDARINI JIJINI DAR LEO

Image
Moto ukiendelea kuwaka katika Makontena yaliandaliwa na kujazwa matairi kwa lengo la kufanya mazoezi, ingawa mitaani tayari zilikwisha enea habari kuwa moto mkuwa umeteketeza makontena, Bandarini jijini Dar es salaam leo. Afisa mawasiliano mkuu wa Bandari, Peter Milanzi, akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo ulipotokea moto ambapo alisema kuwa moto huo, ni sehemu ya mazoezi ya wafanyakazi wa Bandari ili kupima uwezo wa wafanyakazi wa Jeshi la kuzima moto na vifaa wanavyotumia wakati wa ajali za moto.  Aidha Peter, aliwaondoa hofu wananchi kwa kusema kuwa Makontena hayo yaliandaliwa na kujazwa matairi na kuyachomwa moto kwa lengo la kufanya mazoezi, ingawa mitaani tayari zilikwisha enea habari kuwa moto mkuwa umeteketeza makontena.  Baadhi ya majeruhi 

Miss Kinondoni Atwaa Taji la Miss Tanzania 2016

Image
  Diana Edward Lukumai akiwapungia mkono mashabiki mara baada ya kuvikwa taji la Miss Tanzania 2016 usiku wa kuamkia leo jijini Mwanza. Miss Tanzania 2016, Diana Edward (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Grace Malikita na wa tatu,  Maria Peter. Warembo walioingia Top 5. Miss Kinondoni 2016, Diana Edward Lukumai aimeibuka kidedea kwa kutwaa taji la Miss Tanzania 2016. Shindano hilo kwa mara ya kwanza limefanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall. Diana ameibuka kidedea na kuwabwaga wenzake 30. Miss Tanzania 2016, Diana Edward Lukumai katika pozi tofauti.