RAIS JOSEPH KABILA WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha
mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mara
baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere JNIA.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na
mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa kabla ya ukaguzi
wa gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya heshima yake.
Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akikagua gwaride la
heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili uwanjani
hapo.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akiangalia kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati
kikundi cha ngoma za asili kilipokuwa kinatumbuiza uwanjani hapo. PICHA
NA IKULU.
Comments
Post a Comment