Diamond Akiri Mimba Ya Mobeto Kuharibika
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.
BAADA ya ukimya wa muda mrefu kutawala kuhusu
ujauzito alionao mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto, Nasibu Abdul
‘Diamond’ ameibuka na kukiri kuwa mimba ya mrembo huyo imeharibika.
Mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto.
Diamond aliyekuwa akitajwa kuwa mhusika wa kiumbe hicho, alifunguka
hayo kupitia Kipindi cha D’ Wikend Chart kinachorushwa na Runinga ya
Clouds mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine
aliyozungumza, alikanusha taarifa za yeye kuwa mhusika lakini akakiri
kwamba mrembo huyo alikuwa mjauzito na sasa mimba imeharibika.“Mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama ana mimba lakini ndiyo hivyo tena imeharibika so yupo kwenye wakati mgumu. Tumpe pole na tumpe pole pia aliyekuwa mhusika wa kiumbe hicho.
Hamisa Mobeto akiwa katika pozi.
Mimi si mhusika bwana, hata wakati tunashuti naye Salome nilikuwa
sijui kama ni mjamzito lakini ndiyo hivyo kwa sasa hatuna budi kumuombea
arudi katika hali yake ya kawaida,” alisikika Diamond. Ijumaa Wikienda
lilimvutia waya Mobeto ili kuweza kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu
hiyo, simu yake iliita bila majibu.Ujauzito wa Mobeto ulikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliamini mhusika ni Diamond kitendo ambacho kilisababisha maneno kumfikia mpenzi wa staa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kutibua hali ya hewa lakini kwa sasa mambo yako shwari baada ya Zari kuelewa kwamba Mobeto hana madhara.
Comments
Post a Comment