MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SARPCCO)
Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akihutubia wakati wa Ufunguzi wa
mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika
(SARPCCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu ambaye amekabidhiwa Uenyekiti wa
Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO)
akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Dos Santos
JANE (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo mara baada
ya kukabidhiana Uenyekiti katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC
jijini Arusha
Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimpa mkono wa pongezi Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti
wa SARPCCO kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za
Kusini mwa Afrika.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni akihutubia kwenye mkutano
wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za kusini mwa Afrika.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka
Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Bara la Afrika kuweka mipango na
mikakati madhubuti ya kukabiliana na vitendo mbalimbali vya uhalifu
vinavyotokea katika ukanda huo kama hatua ya kuhakikisha wananchi
wanafanya kazi zao kwa amani na utulivu.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 16-Sep-2016 wakati anafungua
mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika katika ukumbi
wa mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu
katika kuibua changamoto mbalimbali za kihalifu na kuzifanyia kazi
ipasavyo kwa manufaa ya ukanda huo.
Amesema
ni wajibu wa wakuu hao wa majeshi ya polisi ya kusini mwa Afrika
kujiepusha na malalamiko yasiyo ya msingi kutoka kwa raia ambayo
yanasababishwa na vitendo vya urasimu, uzembe na rushwa ili kujenga
uwazi na uwajibikaji.
Makamu wa
Rais pia amehimiza kudumishwa kwa ushirikiano miongoni mwa wakuu wa
majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika kubadilishana mbinu bora za
kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kuvuka mipaka.
Katika
mkutano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini –IGP- Ernest Mangu
amekabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi
kusini mwa Afrika (SARPCCO) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Nchi
ya Msumbiji Dos Santos JANE.
Shirikisho
la SARPCCO lilianzishwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano
wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya
uhalifu katika ukanda huo.
Shirikisho
hilo linaundwa na nchi wanachama 15 ambapo baadhi ya nchi hizo ni
Angola, Botswana, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-
DCR-,Malawi, Zambia, Zimbabwe, Madagascar,Swaziland, Afrika
Kusini,Lesotho, Syshelles na Tanzania ambayo ni mwenyekiti mpya wa
SARPCCO.
Tanzania
imekabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO wakati ndio Mwenyekiti mpya wa Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika inayojulikana kwa jina la (SADC TROIKA).
Comments
Post a Comment