Lema Apandishwa Kizimbani kwa Kesi Mbili Tofauti, Aachiwa kwa Dhamana
Dar es Salaam.
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema amepandishwa mahakamani leo katika kesi mbili tofauti.
Kesi ya kwanza namba 351/2016
anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa uchochezi Mkuu wa Mkoa Arusha,
Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu tutakudhibiti kama mashoga
walivyodhibitiwa Uarabuni”
Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.
Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali, Vincent Njau kuzuia dhamana kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.
Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani
wakati polisi wanataka kumpeleka Lema magereza kwa madai kuwa wanadhani
wamechelewa, lakini mbunge huyo alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa
mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.
Baada ya kusomewa kesi hiyo, Mahakama ya
Hakimu Mkazi Arusha imemuachia Mbunge wa Arusha, Godbless Lema kwa
dhamana baada ya kulala mahabusu kwa siku tatu bila kula
Comments
Post a Comment