UVCCM WAAHIRISHA MAANDAMANO YAO,WATII AGIZO LA JESHI LA POLISI
Agosti
22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba
ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima
yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija,
ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.
Msimamo
na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio
hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza
awali yaani Agosti 31 mwaka huu.
Jumuiya
yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu
mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi
Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka
UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.
Kwa
mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo
Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM
tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi
wake hakui, hana jeuri wala ubishi.
Mtoto au
watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa
watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu,
hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii
maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu
nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.
Sambamba
na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano
yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa
na maandamano nchi nzima.
Jambo
jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni
taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na
Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza
suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.
Pia jambo
jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za
maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake.
Wanajeshi
wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na
mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si
heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja
wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya
la usafi wa mazingira.
UVCCM
tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya
kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka
na si wakati huu.
Tunaelewa
kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama
tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine
hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali
katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa
masuala ya kiutawala.
Tulishusha
maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya
Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD,
washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama
tulivyokusudia.
Watendaji
wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za
kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi
tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema
kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.
UVCCM kwa
wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita
katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo
ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza
kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo
kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John
Pombe Magufuli kwa vitendo.
Tumewataka
Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na
Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.
UVCCM
tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu
Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe
nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu
kama tulivyotangaza hapo awali.
UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU.
Comments
Post a Comment