Mamia Wauaga Mwili wa Kabwe Dar
MAMIA ya wakazi wa jiji
la Dar es Salaam, wakiwemo viongozi wa serikali na vyama vya siasa
wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, walijitokeza
kwenye viwanja vya Karimjee, Dar, kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam, Mbonea Wilson Kabwe.
Akizungumza katika maombolezo hayo,
waziri Simbachawene aliwapa pole wafiwa kwa msiba huo na kutoa salaam za
rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Magufuli.
”Tumepata pigo kama serikali, hakika
atakumbukwa kwa mema na mchango alioutoa enzi za uhai wake, nitaungana
na wafiwa kuelekea Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya
kumpumzisha mpendwa wetu,” alisema Simbachawene.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, aliungana na ndugu jamaa na marafika katika maombolezo hayo
huku akisema kuwa kwa niaba ya mkoa wa Dar es Salaam anatoa pole kwa
wafiwa.
Mwili wa marehemu, Wilson Kabwe umesafirishwa kuelekea kijijini Mamba Wilayani Same kwa ajili ya mazishi.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
Post a Comment