Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudani Kusini Awasili Tanzania
Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika
ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi
ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit akiongozana na
rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi
Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wa pili
kushoto) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15
Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya
kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (wa tatu kulia) akisalimiana na Kamanda
Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro mara
baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016
Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na baadhi ya
viongozi waliokuja kumpokea mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya
kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe.
Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akipita katikati ya gwaride
la Jeshi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15
Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametia saini mkataba wa nchi yake kujiunga rasmi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kiir ametia saini mkataba huo jijini Dar es Salaam mbele ya mwenyeji wake, Rais wa Tanzania John Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
Viongozi wa nchi za jumuiya hiyo waliidhinisha kukubaliwa kwa Sudan Kusini kujiunga na jumuiya hiyo kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Arusha mwezi uliopita.
Sudan Kusini itakuwa nchi ya sita kujiunga na jumuiya hiyo iliyoanza kwa nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda. Rwanda na Burundi zilijiunga na jumuiya hiyo baadaye.
Baada ya kujiunga rasmi leo, Sudan Kusini inatarajiwa kufungua mipaka yake kwa ajili ya biashara. Tayari kampuni na asasi nyingi za kifedha kutoka Kenya zimefungua biashara nchini Sudan Kusini.
Wengi wanatarajia hatua ya leo itafungua fursa zaidi za kibiashara kati ya Sudan Kusini na nchi wanachama wa jumuiya.
Wadadisi wengine wanaamini kuwa baadhi ya miradi ambayo Sudan Kusini ingetaka kujumuishwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni miundo msingi ikiwemo reli na mabomba ya mafuta.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO

Comments
Post a Comment