MWAKILISHI MPYA WA UNHCR NCHINI AJITAMBULISHA KWA WAZIRI KITWANGA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akimkaribisha
ofisini kwake Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati alipokuwa anawasili
ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kwa Waziri huyo mara baada ya
kuteuliwa na Shirika lake kuja kuiongoza UNHCR nchini. Hata hivyo,
viongozi hao katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali
jinsi wa kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia), akimfafanulia
jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia
Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea
Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha baada ya
kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),
akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi
huyo alipomtembelea Naibu Waziri huyo ofisini kwake kwa lengo la
kujitambulisha baada ya kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika
hilo nchini. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi
nchini, Harrison Mseke. Katikati ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika
hilo, Yoko Akasaka, na Afisa wa Shirika hilo nchini, Daria Santoni (wa
pili kulia).
Mwakilishi
Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR),
Chansa Kapaya (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga wakati Mwakilishi huyo mpya nchini alipomtembelea
Waziri huyo ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya
kuteuliwa na UNHCR kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika
picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (katikati), pamoja na
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Kapaya
ameteuliwa na UNHCR kuwa Mwakilishi wa Shirika hilo nchini na
amemtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha,
hata hivyo katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali ya
jinsi ya kuwahudumia Wakimbizi waliopo nchini.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments
Post a Comment