TTCL Yajivunia Modemu Mpya za Intaneti ya 4G
Afisa Mauzo Mkuu wa TTCL Shop
Mwananyamala, Dar, Bi. Leyla Pongwe (katikati) akielezea namna ambavyo
huduma ya 4G LTE na router mpya ya TTCL inavyofanya kazi, kushoto ni
Afisa Masoko, Bi. Mboka Kategela kutoka Kituo cha Huduma kwa Wateja cha
Mwananyamala na kulia ni Afisa Mauzo, Bw. Chacha Ghati Mosenye
walipofanya mahojiano na Global TV Online leo.Afisa Masoko Kutoka TTCL Extelecom, Samora Avenue -Dar, Bw. Joel J. Goyayi akielezea namna ambavyo modem zao zinavyofanya kazi. Wakisikiliza
swali kutoka kwa mwandishi wa habari wa Global Publishers, Andrew
Carlos (hayupo pichani) kuhusu uboreshwaji wa vifurushi vya intaneti vya
TTCL.Bi. Mboka Kategela (kushoto) akishika modemu ya Mi-Fi wakati Bi. Leyla Pongwe akishika vocha ya TTCL ya Tsh. 5000/=.Wakitambulisha bidhaa hizo kwa wanahabri wa Global Publishers.Wakiwa kwenye picha ya pamoja.Wakisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanahabari.
Maofisa Masoko kutoka TTCl wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers,
Kitengo cha Teknolojia ya Habari.
MAOFISA Masoko kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL wametembelea televisheni ya mtandaoni ambayo ni namba moja nchini, Global TV Online
na kufanya mahojiano maalum ambayo yalikuwa na lengo la kuwajulishwa
Umma wa Watanzania na watumiaji wa huduma za intaneti kuwa, kampuni hiyo
imeingiza sokoni vifaa vya intaneti vinavyotumia na teknolojia ya 4G
yenye kasi zaidi.
Akizungumza kwenye mahojiano hayo, Afisa
Mauzo Mkuu wa TTCL Shop Mwananyamala, Dar, Leyla Pongwe alisema kuwa,
TTCL wamekuja na huduma ya 4G LTE ambayo mtumiaji wake atapata inateti
ya kasi zaidi kwenye data na voice kwa wale waishio jijini Dar es
Salaam.
Mbali na hivyo TTCL wamkuja na vifaa maalum kwa matumizi ya intaneti, baadhi ya vifaa hivyo ni USB Modem inayotumika kwa kompyuta moja, modem ya wireless (Mi-Fi) inayoweza kuunganisha hadi vifaa 10 vinavyotumia intaneti pamoja na CPE router inayoweza kuunganisha hadi vifaa 32 vinavyotumia intaneti pia inatumia wireless na cabling.
Hata hivyo Maofisa Masoko wa TTCL, Joel
J. Goyayi na Mboka Kategela hawakusita kuelezea kuwa, huduma ya 4G kwa
sasa inapatikana Dar es Salaam pekee na bado kampuni hiyo inazidi
kujenga miundombinu ya kufikisha huduma hiyo mikoa mingine ya Tanzania.
PICHA NA HILARY DAUD/GPL
Comments
Post a Comment