Fahamu mbinu 10 za vigogo kusafirisha unga

6Viatu vya kimasai  na zana nyingine zinazotumika kama urembo ambavyo vimetajwa kama zana muhimu zinazotumiwa katika usafirishwaji wa madawa hayo.
Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Tanzania kwenye viwanja vya ndege vilivyopo nchini limekuwa likipambana na wauza madawa ya kulevya ‘unga’ kwa kugundua na kuzima mbinu zote wanazotumia kusafirisha biashara hiyo haramu, hivyo kupunguza kasi ya uingizwaji na utoaji wa unga kwa njia ya ndege, UWAZI limeambiwa.
Akizungumza na gazeti hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika wiki iliyopita Makao Makuu ya Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania yaliyopo jijini Dar, Kamanda wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno  (pichani) alizitaja mbinu kumi wanazotumia wauza unga hao kusafirishia bidhaa hiyo.
“Kwanza napenda kuweka wazi kuwa, kwa sasa hatuna mchezo na wauza unga. Mbinu zao zote wanazotumia kusafirishia madawa yao tunazijua. Na napenda kuchukua nafasi hii kuwaambia wauza unga wote kwamba, hakuna atakayepona safari hii,” alisema Otieno.
1Kiatu cha kimasai kikiwa kimesheheni mzigo.
Akaendelea: “Wamekuwa wakisafirisha unga kwa kuhifadhi ndani ya magogo. Gogo linapasuliwa wanaweka unga humo. Barabarani askari wanajua ni magogo tu. Wengine wanatumia  vinyago. Wangine wanaingiza unga kwenye vipuli vya magari.
Kamanda Otieno akaendelea: “Lakini pia mbinu nyingine kubwa ni kuweka kwenye sendozi za Kimasai. Wanaweka unga katikati ya soli na sehemu ya kukanyagia, kisha wanashona. Wanapokaguliwa, wanasema ni sendozi wanapeleka kuuza mikoani, kumbe katikati kuna unga.  Pia wanatumia hereni nene, kwenye  soksi na bangili nene.
“Sasa hivi kuna mbinu nyingine, wanachukua vitunguu, wanakata na kuondoa nyama za katikati, wanaweka vipaketi vya unga, wanafunika. We ukiangalia hivi unaona vitunguu.
5Moja ya kipuli cha gari kikiwa kimeshindiliwa mzigo wa madawa hayo haramu.
“Pia wapo wanaotumia sabuni za vipande, wanachimba katikati na kuweka unga humo, wanavirudishia na kuviweka kwenye maboksi kama  bidhaa inayopelekwa kuuzwa kwa matumizi ya kufulia. Pia wengine wanatumia pindo za suruali, wanaingiza unga katikati. Mbinu hizo na nyingine kibao tunazijua, wasirogwe.
“Vigogo hao wamekuwa wakijifanya wanasafirisha vitu hivyo wanavyofichia madawa ya kulevya kama biashara lakini kutokana na ujuzi tulionazo pamoja na vifaa na mbwa tumekuwa tukiwakamata. Nina uhakika kuwa biashara hii inazidi kutoweka na ipo siku itakwisha kabisa.”
Kamanda Otineo aliendelea kusema kuwa, ni kazi ngumu kupambana na wauza unga kwani wamekuwa wakibuni mbinu kila kukicha lakini polisi na vyombo vingine vya dola wamejipanga vizuri kuhakikisha hakuna anayepitisha biashara hiyo katika viwanja vya ndege nchini.
Alisema mafanikio mengine yanatokana na ushirikiano wa wananchi hivyo amewaomba kuendelea kushirikiana kwani vita dhidi ya madawa ya kulevya siyo ya serikali peke yake

Comments

Popular posts from this blog