RAIS DKT MAGUFULI NA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME WAZINDUA RASMI DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO NA KITUO CHA HUDUMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja
la kimataifa la Rusumo, mchana huu. Tukio hilo limehudhuriwa na
viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na
Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja
la kimataifa la Rusumo, mchana huu. Tukio hilo limehudhuriwa na
viongozi wa ngazi za juu serikalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na
Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 6, 2016 amezindua
daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha
Rusumo. Zoezi hili la uzinduzi limefanyika kwa pamoja kwa kuwahusisha Rais Mhe. Dkt. Magufuli wa Tanzania na Rais wa
Rwanda Mhe. Paul Kagame, pia tukio hili limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za
juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali
za Kitaifa na Kimataifa.
Daraja la Kimataifa
la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani ni kiungo muhimu katika Ukanda
wa Kati(Central Corridor), mtandao huu wa barabara unaunganisha barabara kuu ya
Dar es Salaam - Chalinze – Morogoro –
Dodoma – Singida – Nzega – Tinde – Isaka – Lusahanga na Rusumo kupitia Kibingo
Nakayonza hadi Kigali Nchini Rwanda. Mtandao huu utakuwa kichocheo kikubwa cha
ukuaji wa uchumi kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda.
Akizungumza katika
sherehe za uzinduzi wa mradi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Magufuli aliwahimiza Wananchi wa Nchi zote mbili kutumia fursa ya uwepo wa
Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani Rusumo
kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Jumuiya yetu Afrika Mashariki kwa
ujumla.
Aidha Mhe. Rais amewaasa Wananchi kulinda miundombinu kwani kuna baadhi
ya wananchi wanadiriki kuiba alama za barabarani, vyuma vya madaraja na
kuharibu taa za barabarani kwa baadhi ya miji, ameagiza vyombo vya usalama
kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria kwa
wale watakaodiriki kufanya uharibifu huo.
Aidha licha ya
mradi huo kurahisha usafairishaji wa bidhaa na watu Kwa upande wake Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa alieleza
faida kadhaa za mradi huo zikiwemo; kuwa ni kiungo muhimu cha kuiunganisha
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Kikanda kama vile SADC na COMESA, kurahisisha mawasiliano ya
kijamii baina ya watu wa Tanzania na Rwanda, pamoja na kuimarisha uhusiano na
kukuza biashara kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda na Nchi nyingine
za Maziwa Makuu.
Ujenzi wa Daraja la
Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi
inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na
Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA.
Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka.
Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka.
Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi
wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo
limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote
mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na
Kimataifa.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa hu.
Comments
Post a Comment