Mwisho mwampamba kortini

DSC_5699Mwisho Ephraim Mwampamba akiwa Mahakamani.
NA Dustan Shekidele, RISASI mchanganyiko
MOROGORO: Ikiwa takriban siku 40 tangu baba yao, Dk. Ephraim Njawala Mwampamba, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) afariki dunia, mwanaye Mwisho Ephraim Mwampamba ameburuzwa mahakamani na kaka yake, Robert Ephraim Mwampamba, Jumatatu iliyopita.
Kesi hiyo namba 197/2016 ilisikilizwa katika  Mahakama ya Mwanzo Chamwino iliyopo Mazimbu mkoani hapa, ambapo Robert alimburuza mahakamani hapo mdogo wake huyo waliyechangia baba, akimtuhumu kumtukana matusi ya nguoni huku sehemu kubwa ya matusi hayo yakiwa ya kibaguzi.
DSC_5698Robert Ephraim Mwampamba anayedaiwa kumbuluza Mwisho mahakamani.
Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwisho alitokea mahabusu alikolala kwa siku moja ambapo baada ya kesi kusikilizwa, alipata dhamana huku ikidaiwa kuwa kesi hiyo imemkalia vibaya kutokana na ushahidi unadaiwa upo.
Akisoma kesi hiyo mahakamani hapo, Hakimu Amina Chungulu alidai Mwisho anatuhumiwa kumtukana matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia namba za simu (tunazihifadhi) ambayo inaaminika inamilikiwa na Mwisho Mwampamba.
Mwisho alipoulizwa na hakimu huyo alikana kutenda kosa hilo na Robert alipoulizwa kama ana ushahidi ndipo aliposema anao wa meseji hizo kwenye simu yake.
DSC_5695(1)…..Akiwa kwenye gari la polisi.
Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 11, mwaka huu huku Robert akitakiwa kufika mahakamani hapo na meseji hizo kama ushahidi.
Aidha, Hakimu Amina alisema dhamana iko wazi kwa mshitakiwa; mdhamini mmoja na shilingi laki 4 ambapo kaka mwingine wa Mwisho aliyezaliwa naye baba mmoja na mama mmoja, lsambe alimdhamini mdogo wake huyo.

Comments

Popular posts from this blog