Mkurugenzi Manispaa ya Ilala aahidi kuisafisha Dar



    1
Baadhi ya magari yanayotumika kuzoa taka  yakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja .
2 Mwonekano wa baadhi ya magari ya makampuni yanayozoa uchafu katika Manispaa ya Ilala jijini Dar.
3 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi,  (wa kwanza kushoto) akikagua baadhi ya vifaa vinavyotumika kufanyia usafi.
4 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni binafsi inayojishughulisha na kufanya usafi wakiwa mbele ya vifaa vyao vya kazi baada ya ukaguzi.
5.
6Mngurumi (wa pili kushoto) akizungumza jambo mara baada ya ukaguzi.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Isaya Mngurumi,   amesema atahakikisha kuwa jiji la Dar linakuwa safi na lenye kuvutia.
Hayo ameyasema leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar alipokuwa akifanya ukaguzi wa  vitendeakazi  vinavyotumiwa na makampuni binafsi  kusafisha mazingira yaliyopo ndani ya wilaya yake.
Mngurumi  amesema kila kampuni iliyochukua tenda ya kufanya usafi  ihakikishe ina vifaa vya kutosha ambavyo ni kama vile magari ya kuzolea taka, mifagio  na vifaa vingine huku akisisitiza kuwa atakayekiuka makubaliano ya mikataba yao hatasita kuivunja.
Mngurumi alikagua baadhi  makampuni sita yaliyokuwa yamepeleka magari yao yanayotumika katika zoezi zima la kubebea taka zinazokuwa zimekusanywa katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri.
Zoezi hilo limefanyika kulingana na alivyokuwa amewaagiza wamiliki wa makampuni hayo, ambapo pia kwa mujibu wa kiongozi huyo alisema zoezi hilo ni endelevu la kukagua vitendea kazi kila baada ya miezi mitatu.
Na Denis Mtima/Gpl



Comments

Popular posts from this blog