KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM KUANZA KAZI HIVI KARIBUNI
Rais Dk. John Pombe Magufuli akikagua kivuko cha MV Dar es salaam.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kivuko
cha Mv Dar es Salaam maarufu kama kivuko cha Rais Magufuli kipo katika
matengenezo ya kawaida na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kama kawaida
siku za hivi karibuni.Akitoa
ufafanuzi juu ya madai ya kutelekezwa kwa kivuko cha Mv Dar es Salaam
katika maegesho yaliyopo kigamboni Jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Manase Le-Kujan
amesema sio kweli kwamba kivuko hicho cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa
bali kimepumzishwa kutokana na matengenezo yaliyohitajika kufanywa
katika kivuko hicho ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa
wasafiri.
“Sio
kweli kwamba Kivuko cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa katika maegesho
ya Kigamboni bali kimepumzishwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo yake
ya kawaida, hii ikiwa ni juhud
i ya kukiwezesha Kivuko hiki kuwa katika ubora unaotakiwa katika kutoa hudumazake”
“Mbali
na matengenezo pia kuwepo kwa upepo mkali katika kipindi hiki cha mvua
zinazoendelea imetufanya tukipumzishe kwa muda kivuko hicho” Alisema
Mhandisi Manase.
Akifafanua
zaidi,Mhandisi Manase amesema kuwa wapo katika mchakato wa kukipeleka
kivuko hicho kwa ajili ya matengenezo makubwa Mjini Mombasa ili
kukiongezea mwendo kasi na uhimili wake ili kiweze kuendana na
mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika usafirishaji kwa kutumia
vivuko na kuhuimili mabadiliko ya hali ya hewa.
Aidha
amesema hakuna mvutano wa watendaji wakuu TEMESA wala madai yoyote ya
kukisimamisha kwa makusudi kivuko hicho bali ni mpango wa TEMESA katika
kukiboresha ili kiweze kuhudumia wananch iipasavyo.
Kivuko
cha Mv Dar es Salaam hufanya safari zake za kusafirisha abiria kutoka
Dar es Salaam kwenda Bagamoyo ikiwa ni juhudi za serikali za kupunguza
tatizo la usafiri wa majini na kwa sasa kimesimama kwa muda kwa ajili ya
matengenezoambayo yakikamilika kitaendelea kutoa huduma kama kawaida.
Ufanisi
wa kivuko hiki utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Bagamoyo,
Mbweni, Ununio, Boko,Bunju, Kunduchi na Msasani wanaofanya safari zao
kwenda Posta nakurudi sehemu wanakotokea. Na pia kitapunguza msongamano
wa magari katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwani baadhi ya watu
wataacha kutumia magari yao binafsi na kupanda kivuko hicho.
Comments
Post a Comment