Wasira: Nilianza kupigwa picha tangu natoka chooni, nahisi huyu katumwa


Mwanasiasa mkongwe na Waziri wa zamani wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira ameeleza sababu zilimpelekea kugeuka mbongo na kutaka kumgonga na gari mwandishi wa habari aliyekuwa anampiga picha.
Wasira ameeleza kuwa alipandishwa hasira na kitendo cha mpiga picha, Michael Samson kumpiga picha nyingi zisizo na idadi huku akimfuata kila anapoenda, punde tu alipotoka msalani.
“Nilianza kupigwa picha wakati natoka chooni tukiwa pale Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza. Nikamuuliza yule kijana, ‘hizi picha zote unanipiga ni za nini?’ akananiambia ni za habari. Nikamuuliza picha zote hizo mia ni za habari? Yeye akaendelea tu kunipiga picha,” Wasira ananukuliwa na gazeti la Mwananchi.
Wasira alikutana na tukio hilo katika jengo la Mahakama ya Biashara jijini Mwanza baada ya kutoka Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza, alipokuwa akifuatilia rufaa yake ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Bunda Mjini yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema).
Mwanasiasa huyo mkongwe alijaribu kumgonga na gari mpiga picha huyo ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la mwananchi baada ya kushindwa kumpokonya kamera yake.
Wasira alieleza kuwa anahisi kijana huyo ametumwa na mahasimu wake kisiasa kwani anaamini bado kuna fitna za uchaguzi

Comments

Popular posts from this blog