BREAKING NEWS : MOTO NWA MAGUFULI WATUA KINONDONI,VIGOGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni, tarehe 02/02/2016
imewafikisha washitakiwa wafuatao mahakamani:-Bw.Bryceson Kajigiri
Mwangoma mwenye umri wa miaka 54, Bw.Abel Sebabil Slaa mwenye umri wa
miaka 44 na Bw.Bernard Thomas Mkude mwenye umri wa miaka 42 kwa kuiibia
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tsh.33,681,780.
Washitakiwa
hawa Bw.Mwangoma na Bw.Slaa wakiwa Maafisa watendaji wa Kata ya Kimara
kwa vipindi tofauti, na Bw.Mkude akiwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kimara
Baruti walitenda makosa kinyume na kifungu cha 31, 22, 28 (1) 3 vya
sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 pamoja na
kifungu cha 258, 270 vya sheria ya Kanuni za Adhabu. Washitakiwa
wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kujipatia manufaa kwa kufanya
wizi wa fedha hizo zilizokua zimewekwa na Wananchi katika akaunti ya
Urasimishaji Ardhi kata ya Kimara iliyopo benki ya Wananchi wa Dar – es-
Salaam (DCB) tawi la Magomeni kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao.
Mshitakiwa
wa kwanza Bw. Mwangoma akiwa mtendaji wa kata kwa kipindi cha tarehe
01/04/2011 hadi tarehe 30/11/2011 kwa kushirikiana na Mshitakiwa wa tatu
Bw.Mkude ambaye ni mshitakiwa wa pili walitumia madaraka yao kwa
kushirikiana kuiba kiasi cha Tsh. 24,764,280. Bw. Slaa akiwa mtendaji
kata kwa kipindi cha tarehe 01/06/2013 hadi tarehe 31/01/2014 kwa
kushirikiana na Bw.Mkude waliiba kiasi cha Tsh. 8,917,500.
Washitakiwa
walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kufunguliwa kesi namba
51/2016 inayosimamiwa na Mhe. Hakimu Mushi. Watuhumiwa wako nje kwa
dhamana na kesi imepangwa kusikilizwa tena tarehe 16/02/2016.
IMETOLEWA NA MKUU WA TAKUKURU (M) KINONDONI
BENN LINCOLIN
04/02/2016
Comments
Post a Comment