DIAMOND PLATINUMS ZARI THE BOSS LADY WALA SHAVU VODACOM
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa
Vodacom Tanzania, Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa
Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kulia) na
Zarina Hassan(kushoto)wakionesha mabango yenye ujumbe wa jinsi ya
kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”, wakati wa uzinduzi wa
promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Itakayowawezesha wateja wa
mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea
jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( kushoto) na Zarina
Hassan(Kulia) wakionyeshwa tangazo la promosheni ya”Ongea Deilee” kwenye
simu lililofanywa na msaanii wa muziki wakizazi kipya Abdul
Nasibu”Diamond Platinum”( katikati) wakati wa uzinduzi wa promosheni
hiyo leo jijini Dar es Salaam, Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa
mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea
jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto) akiongea na waandishi
wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea
Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1
bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda
Vodacom leo jijini Dar es Salaam,anayeshuhudia kulia ni Balozi wa
Vodacom Tanzania,Nasibu Abdul (Diamond Platinum)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) akiongea na
waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni
ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda
wa saa 1 bure kila siku pindi waongeapo jumla ya dakika 10 Vodaocom
kwenda Vodacom, leo jijini Dar es Salaam,wengine katika picha kutoka
kushoto,Zarina Hassan, Balozi wa Vodacom,Nasibu Abdul (Diamond Platinum)
Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn
Mworia.
SASA
ni wakati wa watanzania kuongea, ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,
mtandao unaongoza nchini wataweza kuongea bure kwa saa nzima!
Kupitia ofa yake maalum kwa wateja ya Ongea Bure Deilee, itakayokuwa
ya miezi mitatu mfululizo, wateja wa Vodacom wataweza kuongea kwa muda
wa saa moja bure kila siku.
Ili kujiunga na ofa hii ambayo haijawahi kutokea nchini, mteja
anachotakiwa kufanya ni kuongea kwa dakika 10 kila siku kwa viwango ya
malipo vya kawaida na hapo hapo atapata ofa ya kuongea kwa muda wa saa
moja bure.
Ofa hii ya Ongea Bure Deilee pia imemuhusisha mwanamuziki nguli wa
muziki wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, ambaye moja ya kibao
chake kinachotamba ni ‘Number One’, ambao pia ni mwito wa simu maarufu
kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom
Tanzania Bw. Ian Ferrao amesema “Ongea Bure Deilee ni ofa ya aina yake
kutolewa kwa wateja wa Vodacom popote walipo nchini. Ofa hii imebuniwa
kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya
kuwa murua!”
Aliendelea kusema kuwa Vodacom Tanzania imedhamiria kuendelea kuvuka
kile ambacho wateja wake wanakitarajia, kwa kuwaunganisha kwa viwango
nafuu ambavyo wanazoweza kuvimudu, lengo kubwa likiwa ni kuweza kuwainua
kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Ofa hii itatolewa kwa wateja milioni moja wa kwanza watakaojiunga
kila siku kupitia ujumbe mfupi wa maneno ambapo watakuwa huru kuongea
wakati wowote watakao, iwe usiku au mchana, ili mradi watakaowasiliana
nao ni watumiaji wa mtandao wa Vodacom.
“Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya Maisha ni Murua ambayo jitihada
zetu katika kuwaletea wateja ofa za kipekee na ambapo kupitia ubunifu
wa kutumia mtandao, tunawezesha maisha ya wateja wetu wote nchini kuwa
murua. Kama ambavyo tunasema siku zote, tutaendelea toa huduma
zinazowawezesha wateja wetu kuwasiliana kwa urahisi na wapendwa wao na
hata katika shughuli zao za uzalishaji mfululizo,” aliongeza Ferrao.
Kwa upande wake, Diamond Platinumz, ambaye sasa ni balozi wa Vodacom
alisema “Ninayo furaha kuwa sehemu ya kampeni hii kabambe kutoka
Vodacom. Nilipopata taarifa kwa mara ya kwanza kuhusu ofa hii nilipata
mshtuko na kusema dah, Vodacom imeleta tena bonge la ofa, kwa hakika ofa
hii itaniunganisha na washabiki wangu, marafiki, familia na
wafanyabiashara wengine”.
Aliongeza “Nitawaelezea washabiki wangu, familia na marafiki jinsi
wanavyoweza kufanya maisha yao kuwa murua kupitia kampeni hii mpya
kutoka Vodacom. Wanachotakiwa kufanya ili kujiunga na kufurahia ofa ya
Ongea Bure Deilee ni rahisi tu, yaani ni kupiga simu *149*01#.
Comments
Post a Comment