Mgombea Ubunge ‘Aliyetekwa’ Mtwara Apatikana.......Ndugu Wasimulia Tukio Zima, Polisi Wasema Wanachunguza Kama Ni Kweli Au Lilipangwa

Mgombea  ubunge  jimbo  la  Mtwara  Mjini  kupitia  CHADEMA,  Joel Nanauka alipotea  katika  mazingira  ya  kutatanisha  tangu  juzi  na  kukutwa  ametupwa  nje  ya  mlangoni wa jengo la Kliniki/kituo cha afya  hapo  Mtwara.
Ndugu  wa  mbunge  huyo  wameusimulia  mkasa  huo  kama  ifuatavyo:
"Ndugu yetu Joel Nanauka ambaye anagombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CHADEMA, alipotea katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumatatu Tarehe 5/10/2015. Siku hiyo alitoka kwenye shughuli za kampeni akiwa na wenzake na walirudi nyumbani akiwa amechoka.
"Majira ya saa kumi na mbili na nusu, alimtumia mwenzake ujumbe mfupi wa mkononi (SMS) akimjulisha kwamba kuna mtu amekua akimtafuta tangu wiki iliyopita waonena na mchana wa siku hiyo alimfuata ofisi ya CHADEMA lakini hakumkuta, hivyo anakwenda kuonana naye mara moja eneo linaloitwa Mnarani hapa mjini Mtwara. Eneo hilo sio mbali na nyumbani kwao.

"Muda mrefu ulipita bila kurudi nyumbani huku giza likiwa limeshaingia. Tulizana kupata mashaka na ndipo tukaanza kumtafuta kwa simu na ilitushtua zaidi baada ya kuona simu yake haipatikani (imezimwa).

"Jitihada za kuwasiliana na kila ambaye tulidhani angeweza kuwa anajua alipo au kua na habari zake zilifanyika bila mafanikio.

"Tuliwasiliana na viongozi wa CHADEMA jimbo la Mtwara Mjini lakini nao hawakua na habari. Tulipoona muda unazidi kwenda tulitoa taarifa polisi na kwa kushirikiana nao tulimtafuta Joel usiku mzima bila kuonekana.

"Siku ya jana (terehe 6/10/2015) ilipita bila kua na habari zozote za wapi alipo jambo lilitupa hofu ya uwezekano wa kuwa ametekwa. Polisi waliendelea na jukumu lao a upelelezi.

"Asubuhi ya leo (Jumatano tarehe 07/10/2015) majira ya saa kumi na mbili asubuhi, Ndugu Joel alikutwa ametumwa mlangoni mwa jengo la Kliniki/kituo cha afya hapa Mjini Mtwara akiwa hajitambui, amechoka, amechafuka na shati lake limechanika.

"Alipewa huduma ya kwanza na alipoanza kupata fahamu amekua akilalamika kuwa ana maumivu makali ya shingo na mbavu ikionesha huenda alipigwa.

"Hadi sasa hatujui nini kimetokea na Polisi bado hawajatoa taarifa zozote na ndugu Joel yuko chini ya unagalizi wa madaktari katika hospital ya Mkoa wa Mtwara.

"Ikumbukwe jimbo la Mtwara Mjini ni kati ya majimbo ambayo umoja wa wananchi UKAWA hawajafikiana kuteua ugombea mmoja wa Ubunge na hivyo bado kuna wagombea wa vyama vya CUF, NCCR na CDM.

"Siku kama tano zilizopita, Ndugu Joel alitoa kauli kupitia radio mojawapo hapa Mtwara akieleza nia ya kujitoa kugombea Ubunge  kwa maelezo kwamba umoja wao umeshindwa kuafikiana juu ya nani agombee.

"Pia alisema kwamba amekua akifanyia siasa chafu na wenzake na huku yeye mwenyewe na familia yake wakititishiwa maisha.

"Hata hivyo, siku moja baadaye, chama chake kilitoa kauli kwamba hakijamkubalia kujitoa kwenye kinyang'anyiro na hivyo analazimika kuendelea na kampeni.

"Kwa mazingira haya tunaamini kwamba tukio la kutekwa na kuumizwa kwake lina uhusiano na siasa za uchaguzi mkuu na matisho aliyokua ameyapataka kabla ya tukio hili."

Kauli  ya  Jeshi  la  Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe  amesema  kuwa  jeshi lake linachunguza kwa kina taarifa za kutekwa kwa mgombea ubunge jimbo la Mtwara mjini (Chadema) Joel Nanauka na endapo litabaini kuna udanganyifu ameufanya dhidi ya tukio hilo hatua za kisheria zitachukuliuwa dhidi yake.

Akizungumza jana, Mwaibambe alisema wanalichunguza tukio hilo ili kubaini kama kuna ukweli, kutokana kuwapo kwa tetesi zinazoonyesha huenda tukio hilo lilipangwa kutokana na mazingira ya kutoweka kwake hadi kupatikana.

Comments

Popular posts from this blog