MGOMBEA MWENYE ELIMU YA MSINGI APITA KURA ZA MAONI!!..SOMA HAPA


Jimbo la Makambako
ALIYEKUWA mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini, Deo Sanga Maarufu kwa jina la Jah People yupo katika nafasi ya kurudi bungeni baada ya kuibuka mshindi wa kura za maoni za jimbo jipya la Makambako.
Alipokuwa akigombea mwaka 2010, Sanga atakumbukwa kwa namna alivyokuwa akiinadi elimu yake ya msingi kwa wapiga kura wake.
"Mimi ni msomi wa elimu ya juu ya msingi ndio maana ni mfanyabishara mkubwa niliyeajiri wasomi wanaosikiliza maelekezo yangu," hiyo ni moja ya nukuu zake.
Katika kinyang'anyiro hicho, Jah People amezoa kura 7,643 dhidi ya kura 499 alizopata mshindani wake Alimwike Sahwi.
Jimbo la Njombe Kusini:
Vitalis Konga 76, Hassan Mkwawa 152, Mariano Nyigu 86, Alfred Luvanda 978, Arnold Mtewele 1,136, Daniol Msemwa 1976, Romanus Mayemba 2,153 na Edward Mwalongo 3,870.
Ludewa:
Kapteni Jacob Mpangala 205, Zephania Chaula 770 na Deo Filikunjombe 18,290 kabla ya kata tatu za Lifumu, Kilondo na Makonde.
Wanging’ombe
Eston Ngilangwa 47, Abel Badi 106, Nobchard Msigwa 216, Malumbo Mangula 304, Hoseana Lunogelo 322, Kened Mpumilwa 332, Abraham Chaula 382, Richard Magenge 417, John Dugange 466, Yono Kevela 1,819, Thomas Nyimbo 1,871 na Gerson Lwenge 11,322 kabla ya kata tatu za Makoga, Kidugala na Igosi.

Matokeo hayo ni kwa mujibu wa katibu wa CCM Mkoa Hosea Mpagike.

Comments

Popular posts from this blog