BALOZI JUMA MWAPACHU AFUNGUKA MAZITO KUHUSU EDWAED LOWASSA
Kauli ya Juma Volter Mwapachu Kuhusu Lowassa
Nimekuwa
kimya kwa muda mrefu katika mabadilishano ya fikra kwenye mtandao huu ambao kwa
hakika, kwa maoni yangu, haubidi kuwa ni wa fikra pevu zisizo shawishika na
misimamo ya 'kimalaya ya siasa'.
Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.
Kama tutaserereka katika msingi huu, basi ni bora Chambi ukafunga virago na kusitish huu mtandao. Nimesoma mabadilishano na mabishano ya fikra kuhusu hali ya siasa nchini mwetu na hususa ni baada ya Mhe Lowassa kuamua kujiunga na Chadema na kuwa mwakilishi wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano. Sijui nyie wenzangu mmesimamia wapi katika suala hili.
Naomba
niseme mwanzoni kabisa kwamba nchi yetu hii leo imefikia mahali ambapo wasomi,
wanazuoni kama sisi katika mtandao huu, Hatuna budi kujitokeza na kuhesabika
tunamuunga nani mkono katika uchaguzi ujao wa Rais wa Tanzania. Tuwe wakweli na
siyo kuendelea kuegemea katika kificho cha 'uhuru' wa wanazuoni katika kutoa
maomi na fikra kama vile sisi si wapiga kura au wananchi wanaothamini umuhimu
kuhusu uongozi wa nchi yetu. Wakati huo umepitwa na hali halisi ya itikadi na
maana muhimu ya uongozi wa Taifa.
Sasa,
Mimi
binafsi, namuuunga mkono Edward Ngoyai Lowassa. Yako mengi ambayo
kazuliwa
huyu ndugu yetu; tunaambiwa tangu 1995 wakati Mwalimu Julius Nyerere
alipotamka kwamba 'huyu kijana ninalo faili lake, ana utajiri
usiyoelezeka. Ana
nyumba kadhaa.' Lakini huyo huyo Baba wa Taifa alimpenda sana Edward na
kumpa
madaraka ndani ya CCM na baraza la mawaziri. Kama Edward alikuwa
'corrupt' swali
ni kwanini Baba wa Taifa hakumchukulia hatua za kisiasa na kisheria?
Kwanini
aseme hayo aliyoyasema mwaka 1995 wakati Edward Lowassa alikuwa
akiongoza
kupendwa dani ya CCM, ngazi zote na akitarajiwa ndiye angependekezwa
kuwa mgombea wa Urais? Jamani, wanazuoni, lazima mtafakari historia na
hali halisi
ilivyokuwa. Mhe Jakaya Kikwete hakuwa 'the favourite' candidate in 1995.
Na
Mwalimu alimtaka Ben Mkapa wakati ule awe Rais. Ilibidi Lowassa atoswe
kinamna!
Mimi
namfahamu Edward, Ninyi mnaujua huo utajiri wake au basi akitoa michango hapa na
pale ni pesa zake? Kati yenu mna utajiri zaidi ya Edward. Edward alivumilia na
kumsaidia mwenzake (nasita sasa hivi kutumia neno 'rafiki') Jakaya ashinde
uteuzi wa mgombea wa CCM hapo 2005. Aliamua hivyo baada ya makubaliano ya 1995.
Wapo wengi wa Tanzania waliyojitolea muhanda, wa hali na mali kuungana na
Edward kumwezesha Jakaya Kikwete kuwa Rais 2005. Kati yao, ndiyo wamekuwa
karibu na Edward katika kinyang'anyiro cha majuzi Dodoma. Imani yao ilikuwa
kwamba pamoja na mkanganyiko wa Februari 2008 wa Richmond ambao hauna mashiko
yoyote ya ufisadi kwa maana ya rushwa, Rais Kikwete angemfungulia mlango
mwenzake Edward kuwa mgombea wa CCM. Badala yake Edward bado akajengewa mzengwe
wa utajiri kama Baba wa Taifa alivyofanya 1995. Hivi leo tukichambua nani kati
yetu ni tajiri zaidi ya Lowassa tutakuwa na viongozi wanao kidhi mategemeo
yetu?
Kuhusu
hili swala la Richmond: Hivi baada ya taarifa ya Tume ya Bunge ya Dr Mwakyembe,
Serikali ilitoa majibu. Mbona kwenye tuhuma za Bunge kuhusu Tegeta Escrow
imekuwapo taarifa toka kwa Chief Secretary kuhusu suala hilo? Nani aliyejaribu
kutoa maelezo ambayo yangemfungisha Lowassa au kumkomboa kwa kitendo chake cha
kujiuzuru kisiasa? Badala yake, wanazuoni wenzangu ambao sidhani kama tunazo
facts za kutosha tunaendelea kumshutumu Lowassa na kumwona kama vile ni
corrupt na kiongozi asiyefaa. It is not fair.
Mimi
simlaumu Lowassa kujitoa CCM. Ni haki yake na kajieleza vipasavyo kuhusu
maamuzi yake. Je, ni uamuzi wa uroho kuhusu Urais? Jamani, wanazuoni, hivi
kweli tumefikia hatua ya kumwona mtu ana uroho wa Urais? Ili awe au afanye nini
ambacho sisi tufunge macho, na siyo tu kutoona, bali pia kuto chukua hatua?
Ikifikia hapo, basi hatuna Taifa tena!!
Taifa
letu limebahatika kufika hapa lilipofika mwaka huu. Wengi hatukutarajia kwamba
yale ambayo tumekuwa tukitafakari na hata kusali ghafla yameibuka. Sidhani na
siamini kwamba ramani ya siasa ya Jamhuri yetu itabaki ilivyo ifikapo Desemba
2015. Ni ishara ya kheri na mwelekeo mwafaka kwa demokrasia ya Taifa
letu.Naamini kwa dhati kabisa kwamba Edward Lowassa atakuwa kiongozi ambaye
atasaidia ramani hii kuwba na muono mpya.
Juma Volter Mwapachu.
Source: rahatupu
NINI MAONI YAKO KUHUSU HILI NDUGU MDAU WETU ?
Comments
Post a Comment