LOWASSA AZIDI KUVUNJA REKODI YA WADHAMINI, APATA 9516 MKOANI TABORA LEO


Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wana CCM 9516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea majina kutoka kwa Naibu Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Bi. Hidaya Rashid yenye idadi wanachama wa CCM 9516 waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mji wa Tabora, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Mzee Juma Nkumba, aliewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tabora miaka ya nyuma.

Comments

Popular posts from this blog