OFFICIAL : MAN UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA MEMPHIS DEPAY NA KUMPA JEZI

MEP
Klabu ya Manchester United imetangaza  rasmi kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Uholanzi,  Memphis Depay na kumsainisha mkataba wa miaka minne.Mpango wa kumsajili kinda huyu mwenye miaka 21 ulikamilika mwezi uliopita, lakini sasa dili limekamilika rasmi ambapo United imelipa ada ya uhamisho ya  paundi milioni 25.
Kiungo huyo anajiunga na Manchester United kutokea klabu ya PSV Einhoven ambapo alionesha kiwango cha juu kwenye ligi ya Uholanzi akifunga magoli 22 msimu uliopita.
Kijana huyo pia ameonesha kiwango kizuri timu ya taifa na wiki iliyopita alicheza mpira mwingi mno Uholanzi ikifungwa 4-3 na Marekani.
Memphis Depay anakuwa mchezaji wa kwanza  kusajiliwa rasmi na Man United majira haya ya kiangazi ambapo Louis van Gaal anatafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi cha kushindania ubingwa msimu ujao.
CHTom8OWIAAsA2-

Comments

Popular posts from this blog