JINSI YA KUPUNGUZA ULAJI SUKARI

Ulaji wa sukari kupita kiasi unahusishwa na kuongezeka kwa unene, uzito kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari cha ukubwani (aina ya pili), magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ini. 
Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, siyo rahisi kufanya tafiti zinazoonyesha kiasi cha sukari anacho kula mtu kwa siku.


Kwa hiyo, hatuna budi kutumia takwimu za nchi zilizoendelea kama Marekani na ulaji wa watu wake haupishani sana na baadhi ya Watanzania wanaoishi mijini. Baadhi ya tafiti za miaka ya 2008-2009 zinaonyesha kuwa nchini Marekani mtu mzima kwa wastani anakula sukari vijiko vya chai 22 kutoka katika vyakula vilivyosindikwa kiwandani.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimarekani ya Mambo ya Moyo (Aha), kwa watu wazima, wanawake, matumizi yao ya sukari inayotokana na vyakula vilivyosindikwa kiwandani, yasizidi vijiko sita vya chai kwa siku. Kwa wanaume wasizidishe vijiko tisa kwa siku. Watu wafahamu kila gramu nne za sukari ni sawa na sukari iliyojaa katika kijiko kimoja cha chai. Huwa inasisitizwa maelezo katika vyakula vilivyosindikwa viwandani yawe kwenye kifungashio cha bidhaa.

Sukari ni chanzo muhimu cha nishati mwilini.
Bila sukari hakuna uhai. Kuacha kabisa kula vyakula vya wanga na vyenye sukari unaweza kusababisha mwili kuwa na kiwango kidogo sana cha sukari na kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo na viungo vingine. 
Hali kama hiyo ikiendelea, mtu aweza kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu na hata kifo. Hata hivyo, sukari nyingi ni sumu na inadhuru afya. 

Ulaji wa sukari kupita kiasi unahusishwa na kuongezeka kwa unene, uzito kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari cha ukubwani (aina ya pili), magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ini. 

Hatua ya kwanza ya kupunguza ulaji sukari ni kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu hatari ya kiafya inayotokana na ulaji wa sukari nyingi. 

Matumizi ya sukari yanamfanya mtu awe anapenda sukari kama wale walio athiriwa na dawa za kulevya. Watu waache kutumia sukari hatua kwa hatua mpaka ulimi wao uzoee kutumia vyakula vyenye sukari kidogo au havina sukari kabisa. 

Hatua ya pili ya kupunguza ulaji sukari ni kubainisha chanzo kikubwa cha sukari katika vyakula na vinywaji unavyotumia kila siku. 
Unakunywa kwa wingi juisi za viwandani, soda au vinywaji vingine vitamu? Jambo jingine ni kama unaweka sukari nyingi katika chai au kahawa na unakula vyakula vyenye sukari kama keki, mikate ya kumimina au visheti?
Chunguza pia kama una kawaida ya kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukari ama wanga. Mfano kilichotokana na unga wa mahindi yaliyokobolewa. 

Baada ya kujua chanzo kikuu, weka mpango wa kupunguza ulaji wa vyakula hivyo. Kama unaweka vijiko vinne vya sukari katika chai au kahawa, punguza hatua kila wiki kijiko kimoja. 

Baada ya wiki tatu utakuwa unakunywa chai na kuweka kijiko kimoja cha sukari. 
Kama unakunywa soda kila siku chupa tatu, asubuhi, mchana na jioni. Punguza iwe chupa moja kila siku. Baada ya wiki moja punguza mpaka uweze kunywa chupa moja ya soda kila baada ya siku mbili na baadaye uweze kunywa soda chupa mbili kwa wiki.
Halafu jitathmini je, unaweza kuishia hapo au kuacha kabisa na kunywa vinywaji mbadala? kiasi cha sukari anacho kula mtu kwa siku.

Comments

Popular posts from this blog