PENNY: NATAMANI MTOTO, SINA WA KUZAA NAYE
Stori: Imelda Mtema
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.
Penny alitoa tamko hilo baada ya Diamond kunukuliwa jana (Alhamisi) na
gazeti dada la hili, Amani kuwa, alimpa mimba mara mbili binti huyo
lakini zikayeyuka katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Penny alisema, sasa hivi anapomuona
mtoto anachanganyikiwa na kujikuta akitamani naye kuitwa mama hivyo
akimpata mwanaume sahihi wa kutimiza ndoto yake hiyo hatafanya ajizi.
“Kiukweli sasa ndiyo ule wakati wa kuzaa, natamani sana mtoto lakini
sasa wa kuzaa naye yuko wapi? Hapo ndiyo tatizo maana siyo kuzaa na mtu
ili mradi mtoto awe na baba,” alisema Penny.
Comments
Post a Comment