MUONGOZAJI MAHIRI WA FILAMU NA VIPINDI TANZANIA GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI MOROGORO
George Tyson enzi za Uhai wake
Taarifa
zilizotufikia katika meza yetu ya habari Usiku huu ni kuwa Muongozaji
mahiri katika Tasnia ya Filamu Nchini na Mzazi Mwenza wa Msanii Nguli wa
Filamu nchini Vyonne Cherry Au Monalisa, Bwana George Tyson amefariki
Dunia mara baada ya kupata ajali ya gari Mkoani Morogoro Katika Eneo la
Gairo wakati wakitokea Mkoani Dodoma ambapo walienda kwaajili ya
Kuadhimisha Miaka Miwili ya Kipindi Cha Mboni Show.
Bw Tyson
Mauti yamemfika mara baada ya Gari walilokuwa Wakitumia kusafiria Kutoka
Mkoani Dodoma Kupasuka Matairi na kupelekea Kupoteza maisha na
kupelekea hali ya watu wengine wanne waliokuwemo katika Gari hilo kuwa
mbaya baada ya Kuumia vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa
Morogoro kwaajili ya Matibabu.
Ajali hiyo imetokea majira ya Saa Moja Usiku katika Eneo la Gairo
Tutaendelea Kupeana taarifa zaidi kadri tunavyozipata
Tunapenda
kutoa Pole kwa Mmoja wa Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents
ambae ni Mzazi Mwenza wa Marehemu George Tyson, Bi Vyonne Chery Kwa
kuondokewa na Mzazi mwenzie ambae walibahatika Kupata Mtoto Mmoja
aitwaye Sonia.
Comments
Post a Comment