JE UNA FURAHIA KAZI YAKO KAMA ZAMANI? JIFUNZE HAPA NJIA TISA(9) ZA KUIFURAHIA TENA KAZI YAKO KIKAMILIFU

Je unafurahia kazi yako? Kama sivyo basi ni wale watu ambao wamesahau sababu ya kufurahia kazi yao kama mara ya kwanza.Lakini labda ni si kazi yenyewe lakini tatizo likawa mtazamo wako kuelekea tatizo au changamoto. Je, inawezekana kwamba kazi imekudhoofisha kiasi kwamba umeshindwa kuhudumia mahitaji ya msingi au kuyachukulia kwa uzito wa hali ya juu. Umekuwa ukisingizia au kuwalaumu kazi yako? Je, si ni wakati wa kuanza kufurahia kazi yako tena?

Kuna njia tofauti ya kuanza kufurahia kazi yako badala ya kuona kama stress( msongo wa mawazo).
Hebu tuangalie baadhi ya mbinu kwa ajili ya kufurahia kazi yako.

1. Kuendeleza tabia chanya au mtizamo chanya
Hiyo ni pamoja na kuwa na ufahamu wa mawazo yako hasi na kupambana na changamoto hiyo. Kama unawasilisha mchanganuo wa mradi, je mawazo yako yanaingilia utendaji wako, kwa mfano ‘je wataniona sijiamini? Kama ni hivyo kuyasaidia mawazo yako na mawazo muhimu na ukweli kwamba kila mtu ujihishi kutojiamini wakati wao wa kutoa mada au kuwasilisha jambo fulani – Hivyo ni kawaida! Jipange ondoa wasiwasi na angalia kile unachowasilisha! weka ya akili yako katika hali ya kujiamini na kufanikisha jambo.

2. Zikabili Changamoto
Wakati fulani sisi wenyewe huwa na wasiwasi na kutafuta kuepuka changamoto kwa sababu ya wasiwasi na mashaka. Hata hivyo tumekua katika hatua rahisi rahisi inayopunguza na kusababisha kufanya mambo kidogo kidogo. Hivyo ni muhimu kuendelea mbele na kujaribu mambo mapya, licha ya usumbufu. Unaweza kusimama na kuyakabiri!


3. Fanya Kazi kwa kudhibiti hali yako vizuri
Wengi wetu tunashida na udhibiti wa mambo fulani kwa kiwango cha juu hii ni kutokana na kuwa na hali ya kutojiamini na kuhisi kuonewa. Hivyo imesababisha kuwa na tabia ngumu zisizobadilika katika mawazo na ufanyaji wa kazi fulani fulani, imesababisha tuwe ni watu wagumu kuishi au kufanya kazi na wengine. Tumekuwa watu wa kuhukumu mambo kabla hatujayatizama kwa kina.

Unatakiwa wewe mwenyewe uwe na moyo wa subira, inachukua muda kubadili tabia ya muda mrefu. Ukidhamilia kubadilika taratibu utaanza kupata urahisi wa kufanya kazi na watu.

4. Angalia Jambo kwa ukubwa au kwa mtizamo wa mbali kuliko mazingira ya kawaida
Hiyo inamaanisha kuwa makini kuangalia na kutizama jambo kabla halijakughoofisha na mwonekano wake. Jambo linapotokea jaribu kurudi nyuma angalia makusudio yake yalikuwa ni nini au vipaumbele vyake vilikuwa ni vipi? Jiulize matumizi bora ya muda wangu kwa sasa yakoje?

5. Kuwasiliana kwa uthubutu
Hisia na wasiwasi juu ya makosa ya kupindukia au wasiwasi kuhusu jinsi ulivyochukulia jambo fulani linakusababishia wewe kutowasiliana ipasavyo. Lakini kwa kufanya kazi kwenye mlengo chanya wa akili utaanza kuhisi hali ya kufanya kazi kwa kujiamini. Mara baada ya kuanza kusema ‘hapana’ wakati unahitaji kusema hapana, utagundua kwamba, hakuna kitu cha kutisha kinachotokea! Hivyo fikiri namna ya kutenda tofauti, na polepole unaanza kupata matokeo mazuri.


6. Jipange Sawa Sawa
Hakikisha unajua kitu gani kiko mbele yako. Je kuna mkutano ambao unahitaji kujiandaa kabla? Jiandae vilivyo, hakikisha una nyaraka muhimu na kuwasili eneo la mkutano kwa wakati. Na anza kufanya juhudi za kimakusudi kwa ajili ya kupata kasi ya mkutano.


7. Jihadhari usiwe mtu mwenye madai/mategemeo makubwa na kuhukumu wengine
Kama unaweza kukabiliana na hili unatakiwa kujitahidi kuwa na uhalisia wa mambo na busara ya kukabiliana nayo. Sisi sote tuna kasoro (wewe pia)kama unaweza kujirekebisha vivyo hivyo utaona wengine wakijirekebisha na kuanza kushirikiana na wewe.


8. Uwe mwaminifu wewe mwenyewe
Kama unashindwa kujidhibiti na hisia mbalimbali kutoka kwako ( hasira, chuki, hatia au kujihisi mkosaji, wasiwasi, mashaka,huzuni au kushuka kimawazo n.k) Jiulize hasa kitu gani kinaendelea kwako. Siku zote kuna namna ambavyo tunaweza kurekebisha na kuboresha mambo, kama kuna kitu chochote basi kishughulikie na tafuta ufumbuzi wa jambo hilo. Kama kwa upande mwingine huwezi kujidhibiti kubaliana na hali hiyo, kwani unaweza kudhibiti vitu ambavyo vinadhibitika.

9.Uwe mwema kwako mwenyewe
Katika hali zote weka usawa kati ya kazi na maisha ya nyumbani. Hakikisha kuwa na muda wa kupumzika kujirusha na kufurahi maana unahitaji hivyo.Kama umefanya makosa kazini au nyumbani jifunze na uendelee mbele. Jikubali vile ulivyo ingawa ni changamoto lakini unathamani ya kusonga mbele hivyo hivyo. Kumbuka jambo baya linalokusumbua katika maisha yako , na ujisukume kuelekea kuwa mtu kamili mwenye mafanikio.
Je hapo juu kuna baadhi ya maeneo ambayo ungependa kufanya maboresho? Yatambue na uanze kuyatatua sasa. Au tafuta mtu anayeweza kukusaidia katika hali hiyo na kuweza kukufuatilia ufanye mabadiliko hayo.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK KUPATA HABARI ZAIDI NA PIA TUPE MAONI NA USHAURI WAKO 

Comments

Popular posts from this blog