LIBYA MABINGWA CHAN 2014
TIMU ya taifa
ya Libya imetwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2014 baada ya
kuifunga Ghana kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana Jumamosi
Uwanja wa Cape Town.
Ushindi huo ni sawa na Libya kulipa kisasi kwa Ghana baada ya
kufungwa kwa penalti 7-6 miaka 32 iliyopita kwenye fainali ya Kombe la
Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kipa wa Ghana, Stephen Adams aliokoa penalti mbili za Mohamed Elgadi
na Abdelsalam Omar na kufanya mikwaju mitano mitano ya awali imizike kwa
sare ya 3-3.
Ahmed El Trbi
aliifungia penalti ya sita Libya kabla ya Joshua Tijani kukoa upande wa
Ghana na kuamsha shamrashamra za wafalme wa Mediterranean Knights wa
Libya.
Katika mchezo uliotangulia kusaka mshindi wa tatu, Nigeria iliifunga
Zimbabwe 1-0 na kushinda Medali ya Shaba ya michuano hiyo ya tatu.
Libya inakuwa bingwa wa tatu tangu kuanzishwa CHAN, michuano
inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, wakifuata
nyayo za DRC 2009 nchini Ivory Coast na Tunisia 2011 nchini Sudan.
Chanzo:BIN ZUBEIRY
Comments
Post a Comment