HIZI NDIZO NJIA NA NAMNA YA KUMFANYIA MUMEO AWAHI NYUMBANI!
SIPENDI na wala sitaki kusikia kwani inamkoseshe raha mtoto wa mwenzio, kuku wako mwenyewe kwa nini akushikie manati. Kwa nini uishi na mumeo kama kaka yako? Sipendi na kama unatabia hizi ukome na ukomae.
Ooh! Samahani hata salamu nimesahau kukujilieni hali wote wapenzi wa kona hii najua akina mama pekee hata kina baba kuna mtu mzima mmoja aliniambia akikosa kusoma kona hii hujisikia mgonjwa kwa vile amepata mengi kupitia hapa.
Haya tuendelee na yetu hasa yaliyonifanya nifungue mdomo wangu. Kuna baadhi ya wanawake wenzangu wananiudhi sana kufikia hatua ya kukosa raha, unamuonea haya mumeo au mpenzio mkiwa ndani full khanga sipendi eeeh! Umesikia mwili wako mkiwa faragha si mali yako bali ya mwenzako.
Unauficha una kasoro gani mwenzio anahitaji kuliona umbile lililomvutia likiwa na nguo ameliweka ndani ili alifaidi kwa kuliona live, wewe na mikhanga kutwa kucha hata kujipaka mafuta hujipaki mbele ya mwenzio.
Mumeo amekuwa akihangaika kuutazama mwili wako kama wewe siyo wake, hupendi kufanya mapenzi mchana na usiku unazima taa. Kufanya hivyo ni kumnyima haki ya msingi mpenzi wako. Hauko pale kwa ajili ya kuvua nguo za ndani tu, la hasha mwanamke ni pambo la nyumba unatakiwa ujiachie muda ukifika hasa ukijua mwenzio anarudi toka kazini kujiweka kwako kwa kuvaa upande mwepesi wa khanga tabasamu alitoki mdomoni huwa tiba sahihi kwa mihangaiko na maudhi ya kutwa nzima.
Napenda kukupeni kisa kimoja kuhusiana na tabia ya baadhi ya wanawake kuificha miili yao, kuna jamaa mmoja alioa binti aliyeumbwa akaumbika lakini binti yule alikuwa anamuogopa mumewe kwa kuona kukaa bila nguo mbele ya mumewe kwake ilikuwa aibu kubwa.
Comments
Post a Comment