REGNAND MENGI AJIBU TUHUMA ALIZOZUSHIWA
- Get link
- X
- Other Apps
1. Nafurahi
kwa nafasi ya kuwa nanyi leo kwa kuwa sekta binafsi itapata nafasi ya
kipekee kesho tarehe 16 Desemba 2013, ya kuwa na mkutano chini ya Mhe.
Rais Kikwete kama mwenyekiti.
2. Mimi
binafsi nitapata heshima ya kushiriki kama kiongozi wa sekta binafsi
chini ya TPSF. Lakini limekuwepo tatizo la mambo yaliosemwa na Mhe.
Profesa Muhongo kunihusu ambayo ningependa niyafafanue ili nisiende
kwenye kikao cha kesho zikiwepo fikra kwamba mambo hayo ni ya kweli.
3. Katika tarehe za mwanzo wa mwezi Septemba mwaka 2013 Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema kwamba:
“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”
| |||
4. Ukweli
ni kwamba mimi siyo mbinafsi na pili sijawahi kuomba upendeleo wa
kupewa kitalu cha gesi bali ninapigania Watanzania kwa ujumla.
5. Tarehe
8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni
nani anamiliki migodi ya Tanzania, Mhe. Profesa Muhongo alitoa takwimu
za kunihusu ambazo siyo sahihi.
6. Ukweli
ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja
wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita
mojaya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema.
7. Naomba
nisisitize kwamba mimi binafsi nimeshapata nafasi kubwa ya kujiendeleza
kibiashara. Ukweli ni kwamba ninachopigania leo ni juhudi ya kupanua
wigo ili Watanzania wengi waweze kushiriki kama ilivyo kwenye Sheria
ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004, (National Economic
Empowerment Act, 2004) ambayo inatoa upendeleo maalumu kwa Watanzania
katika rasilimali zao.
8. Ninamatumaini
makubwa kwamba katika mkutano wa kesho ambao utatoa fursa kwa sekta
binafsi kuzungumza na uongozi wa Taifa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Rais
utatuwezesha kupata muafaka wa ni jinsi gani tutashirikiana katika
juhudi za kuwawezesha Watanzania kwenye nyanja mbalimbali za uchumi
wetu.
Dkt. Reginald A. Mengi
Dar es Salaam
15 Desemba 2013
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment